Site icon A24TV News

TRA WAMEJIPANGA VIZURI KUWAHUDUMIA WATU 7 7, MBWANA

Na Richard Mrusha

MWENYEKITI wa Jumuiya ya wafanyabiashara soko la Kariakoo Martine Mbwana amewaasa wafanyabiashara kwenda kwenye maonesho hayo kujifunza kwa wengine.

Aidha amewaasa kufika katika banda la Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ili waweze kuona shughuli zinanazo fanywa na TRA na kuhudumiwa kama wana changamoto zozote.

Mbwana ameyasema hayo katika maonesho ya Kimataifa ya 48 Biashara (sabasaba) jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la TRA.

“Mimi nimekuja hapa,nimetembelea kwenye banda la TRA,wamejipanga vizuri kuwahudumia wananchi hususani wafanyabishara.

“TRA wapo idara zote wanafundisha ,wanajibu na changamoto zote zinazohusiana na TRA zinatatuliwa hapa hapa kwenye maonesho.

Mwisho