Site icon A24TV News

VETA KUWAJENGEA UWEZO WATU WANYE ULEMAVU.

 

Na Richard Mrusha

Katika kuwajengea ujuzi watu wasioona vyuo vya elimu ya mafunzo ya ufundi stadi (Veta) vimeanza kutoa mafunzo kwa jamii hiyo kuwanoa kuendana na mahitaji ya soko la ajira katika karne ya sasa.

Mmoja wa wanafunzi asiyeona katika fani ya useremala, Raphael Mwambalaswa, amekuwa kivutio kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) kutokana na kudhihirisha uwezo wake katika fani hiyo.

Mwambalaswa ambaye pia ni Mhadhiri Msaidizi katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), amesema Veta wanaweza kumsaidia mtu asiyeona kuweza kujitegemea ndiyo maana aliamua kwenda kujifunza.

“Nipo nasoma lakini funzo kwa jamii wajue kwamba haya mambo yanawezekana, ukiwa na ulemavu, huoni, usikii, una ulemavu wa viungo au changamoto nyingine yoyote unaweza ukafanya shughuli kama watu wengine ambao hawana ulemavu.

Amesema Muwatie moyo watu wenye ulemavu waje Veta kupata mafunzo, inawezekana…ulemavu siyo mwisho wa maisha, uelmavu siyo kukosa elimu, siyo kukosa ujuzi wa kufanya mambo,” amesema Mwambalaswa.

Naye Mkufunzi katika Fani ya Useremala Chuo cha Veta Dar es Salaam, Mwalimu Salehe Omary, amesema wana miongozo inayowawezesha kutoa mafunzo kwa watu wenye ulemavu wamekuwa wakiwapa maelekezo ya kuzingatia usalama.

Amesema Moja ya majukumu yetu ni kuhakikisha kila mtu anapata ujuzi awe mwenye uwezo wa viungo au asiye na viungo, nimepata mafunzo ya namna ya kuwahudumia watu wenye mahitaji maalumu Changamoto aliyonayo mwanafunzi wangu Mwambalaswa (asiyeona) kwangu ilikuwa ni kitu kipya.

“Lakini kwa sababu nina utayari haikuwa shida, mwanafunzi wangu pia alitumika kama mwalimu kwa kunipa mbinu za kumfundisha, zimetufanya mimi na yeye kazi yetu kuwa rahisi.

Amesema mwanafunzi huyo alipofika chuoni hapo walitumia siku mbili kumzungusha katika mazingira yote ya chuo kuanzia anapoingia getini hadi katika karakara ya kujifunzia bila kupata changamoto yoyote.
Mwisho.