Site icon A24TV News

VETA YAJA NA TEKINOLOJIA KWA SEKTA YA KILIMO

Na Richard Mrusha

Veta yaja na teknolojia ya kumasadia mkulima kwa ajili ya kutengeza udongo unatolewa msituni kwa ajili ya kuotoshea miche ya bustani na mboga mboga kabla ya kupeleka shambani.

Akizungumza leo julai 6,2024 na waandishi wa habari ndani ya Banda la Veta katakata viwanja vya mwalimu Nyerere kwenye maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara saba saba,afisa ufutiliaji na Tathmini ya mafunzo Veta Muhandisi Joseph
Kimako amesema udongo huo wanaoutengeneza unamchanganyiko wa mabaki ya mpunga na mbolea ya samadi.

Amesema mchanganyiko huo wa udongo wanapouchanganya na huupeleka kwenye mtambo kisha uchemsha maji na majai hayo pindi yanapochemka kwa nyuzi joto mia moja huwekwa huo mchanganyiko ndani yake kwa dakika thelathini na kisha hutolewa na kuachwa upoe ndio upatikana mchanganyiko ulio kamilika wa udogo huo.

Amesema hapo awali udongo huu ulikuwa unatolewa kutokae nje ya nchi na kuuzwa kwenye maduka ya pembejeo hivyo basi Veta wakaamua kuja na teknolojia nyepesi kwa lengo la kumsaidia mkulima kuuandaa huo ndogo kwa kututumia mali gahfi za ndani ya nchi badala ya kutegemea udongo kutoka nje ya nchi.

mkulima unapotaka kulima zao la nyanya unaandaa udogo wako na kuuweka kwenye
Sinia za kuoteshea miche kabla ya kupelekwa shambani,”
Amesema Kimako.

Sababu ya kufanya hivyo ni kuwa ndani ya udogo huo mnavirutubisho vyote vinavyohitajika kwa ajili ya mmea kukua ambavyo vinapatikana kwenye udongo wa msituni, mabaki ya mpunga na samadi ya ng’ombe wenye uwezo wa kusaidia mmea kukua haraka wakati wa uoteshaji,

Mhandisi Kimako amesema tekinolojia hiyo inamiaka miatatu tangu waanze kuitumia na kupitia maonesho mbalimbali ikiwamo Sabasaba na maonesho ya kilimo nane nane wakulima wanaopata nafasi kupitia banda hilo uwapa elimu kuhusu namna ya kuandaa udogo huo waweze kulima na kupata mazao kwa tija.

Mwisho.