Site icon A24TV News

WAZIRI MAVUNDE APIGA MARUFUKU WAMILIKI WA LESENI ZA MADINI KUZITUMIA KUINGIZA WAGENI

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

Waziri wa Madini Mhe Anthony Peter Mavunde amepiga marufuku kwa wamiliki wa Leseni za uchimbaji mdogo wa Madini kuingiza wageni kutoka nje ya Nchi kwenye leseni zao bila kuwa na mikataba au makubaliano yaliyopitishwa kwa mujibu wa Sheria.

Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Jijini Dodoma July 28,2024 wakati akizungumza na Wanahabari kuhusu Mwendendo wa makusanyo ya maduhuri yatokanayo na rasilimali madini Nchini kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 na Katazo la Wageni kuungia kwenye PMLs bila kuwa na makubaliano ya msaada wa kiufundi(TSA).

Na kupiga marufuku kwa Wageni wenye leseni kubwa za biashara ya madini hususan wa madini ya vito kwenda machimboni kukusanya Madini kwani kwa kufanya hivyo ni kupora haki ya ajira ya Watanzania.

Na kusema kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa Wamiliki wa leseni za uchimbaji mdogo wa madini pamoja na wageni kutoka nje ya nchi watakaobainika kukiuka matakwa ya Sheria.

“Nachukua nafasi hii kupiga marufuku kwa wamiliki wa leseni za uchimbaji mdogo wa madini, kuingiza wageni kutoka nje ya nchi kwenye leseni zao bila kuwa na mikataba/makubaliano ya msaada wa kiufundi (Technical Support) yaliyopitishwa kwa mujibu wa Sheria”.

” Pia nichukue fursa hii kupiga marufuku wageni wenye leseni kubwa za biashara ya madini (dealer’s Licence) hususan wa madini ya vito kwenda machimboni kukusanya madini. Kufanya hivi ni kupora haki ya ajira ya Watanzania ambao kwa mujibu wa Sheria,kazi ya kufuata madini machimboni inapaswa kufanywa na Watanzania pekee wenye kumiliki leseni ya “broker”.

“Ndugu wanahabari, Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa wamiliki wa leseni za uchimbaji mdogo wa madini pamoja na wageni kutoka nje ya nchi watakaobainika kukiuka matakwa ya Sheria.Ndugu wanahabari, Katika kumalizia, naomba nitoe rai kwa wawekezaji wote wenye leseni za uwekezaji katika Sekta ya Madini kuzingatia matakwa ya Sheria ya Madini, Sura ya 123. Aidha, Wizara ya Madini itaendelea kuwapa ushirikiano wawekezaji wote wa ndani na nje ya nchi wenye nia ya kufanya uwekezaji wenye tija na kukuza uchumi wa taifa letu kutokana na uvunaji wa rasilimali madini”.

Mbali na hayo pia Waziri ameeleza kuwa kumetokea tabia ya wamiliki wa leseni za uchimbaji mdogo wa madini kuingia makubaliano yasiyo rasmi na wageni wakati leseni za uchimbaji mdogo wa madini zinatolewa kwa Watanzania pekee kwa mujibu wa kifungu cha 8(2) cha Sheria ya Madini Sura 123.

Ndugu wanahabari, Kumetokea tabia ya wamiliki wa leseni za uchimbaji mdogo wa madini kuingia makubaliano yasiyo rasmi na wageni kutoka nje ya nchi na kuwaruhusu kufanya kazi katika leseni zao. Ikumbukwe kwamba, leseni za uchimbaji mdogo wa madini zinatolewa kwa Watanzania pekee kwa mujibu wa Kifungu cha 8(2) cha Sheria ya Madini, Sura 123″.

Waziri ameweza pia kuzungumzia suala la uvunjaji wa rekodi katika ukusanyaji wa maduhuli ambapo amesema Wizara ilikuwa ikikusanya kiasi kidogo cha maduhuli ukilinganisha na sasa kwani ndani ya kipindi kifupi limeshuhudiwa ongezeko la makusanyo ya muduhuli yatokanayo na shughuli za uchimbaji mfano mwaka wa fedha 2023/2024 Wizara ilipanga kukusanya jumla ya Shilingi 882,121,205,00 lakini hadi Juni 2023 Tume ya Madini ilikusanya jumla ya Shilingi 753,815,646,,857.13 sawa. A asilimia 85.45 ya lengo lililopangwa.