Site icon A24TV News

WAZIRI WA ELIMU PROF ADOLF MKENDA AWEKA JIWE LA MSINGI CHUO CHA KISASA CH ATC KAMPASI YA KIKULETWA WILAYANI HAI ATOA MAAGIZO KWA WAKUFUNZI .

Na Geofrey Stephen Arusha .

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema kuwa Mradi wa Kujenga na Kuimarisha Ushirikiano wa Kikanda wa Afrika Mashariki (EASTRIP) ni muhimu kwa kuwa una kwenda kusaidia katika utekelezaji wa mabadiliko ya kielimu ambayo yameaanza kutekelezwa kupitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014, Toleo la 2023 pamoja na Mitaala mipya katika ngazi mbalimbali.

Nombo ameyasema hayo Julai 30, 2024 Mkoani
Kilimanjaro wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Arusha Kampasi ya Kikuletwa Wilayani Hai ambapo amesema kuwa ‘Mradi huo umeshirikisha nchi tatu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jamhuri ya Kenya na Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia ambazo kwa ujumla zinatekeleza mradi kwa kuanzisha vituo vya umahiri kumi na sita (16).

Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa Mradi wa EASTRIP unatekelezwa kuendana na miradi ya kimkakati ya Kitaifa na umetengewa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 75 sawa na shilingi Bilioni 187.5 kwa ajili ya kuanzisha Vituo vinne vya umahiri nchini katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na Chu cha Teknolojia Dar es Salaam ambacho kina Vituo viwili vya Umahiri.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Julai 30, 2024 ameweka Jiwe la Msingi la
Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Arusha Kampasi ya Kikuletwa itakayokuwa Kituo cha Umahiri cha Nishati Jadidifu. Kampasi hiyo inajengwa katika Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro ambapo ikikamilika itakuwa na uwezo wa kuzalisha wataalamu wa Nishati Jadidifu wasiopungua 1,500 kwa Mwaka. Kituo hicho cha Umahiri kinajengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Kujenga Ujuzi na Kuimarisha Ushirikiano wa
Kikanda wa Afrika Mashariki unagharimu zaidi ya Bilioni 36.

Mkuu wa Wilaya ya Hai Mh Amiri Mkalipa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ameishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kujenga Kampasi hiyo katika wilaya ya Hai ambayo itakwenda kuinua Uchumi wa wana Hai na Kijiji cha Chemka kwa kuwa kuna uzalishaji wa mazao ya vyakula ambayo yatatumika katika kulisha wanachuo wa kampasi hiyo.
Wananchi wa kijiji hicho Chemka wamepongeza serikali kwa kupeleka mradi huo mkubwa wa chuo cha ufundi kampasi ya kikukeletwa kwani watanufaika na mradi huo .