Site icon A24TV News

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Julai 09, 2024 amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya King’s Trust International (KTI) Kuimarisha ufundi

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Julai 09, 2024 jijini Dar es Salaam amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya King’s Trust International (KTI) ya Uingereza anaeshughulikia Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw. Andre Harriman na kujadili ushirikiano katika kuimarisha mafunzo ya ufundi.

Akizungumza katika kikao hicho Prof. Mkenda amesema kutokana na maendeleo na mabadiliko ya teknolojia, juhudi za kuwezesha vijana kuwa na ujuzi utakaowawezesha kushiriki kikamilifu katika sekta mbalimbali za uzalishaji ikiwemo viwanda.

“Nimewaambia sisi tunataka kupitia Vyuo vya VETA tushirikiane nao kuimarisha ujuzi katika maeneo mawili, moja kuimarisha ni katika eneo la __Mechatronics_ , tuwafundishe namna ya kuwa mafundi mahiri wa magari hasa yanayotumia vifaa vya kisasa” alisema Mkenda.

Aidha amelitaja eneo la pili kuwa ni ujuzi katikabsekta ya nguo ikiwemo kubuni na ushonaji.

Waziri Mkenda amesema kuna fursa nyingi kwa Vijana wa Kitanzania hivyo tumejipanga kuwajengea umahiri kupitia mafunzo katika vyuo vyetu vya VETA kwa kuzingatia Teknolojia za kisasa na hivyo kuweza kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji ya masoko ya ndani na nje ya nchi.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya KTI Bw. Harriman ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwekeza katika miundombinu na maboresho ya Sera ya Elimu yanayowezesha Wahitimu mahiri.

Amesema Taasisi hiyo iko tayari kushirikiana na Wizara katika maeneo yalitajwa kwa kuwezesha Vyuo vya VETA.

Mwisho .