Site icon A24TV News

araza la madiwani Siha wataka wakulima kusaidiwa kuhusu Wanyama waharibifu wakiwamo Tembo

Na Bahati Siha,

Wakulima wa mshamba ya Leon,Pongo na lairongo Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,wataanza kupewa elimu ya namna ya kukabiliana na Wanyama wanaoharibu mazao yao.

Haya yamesemwa na Afisa maliasili Wilayani humo wakati wa Baraza la madiwani lililofanyoka katika ukumbi wa halmshauri hiyo ,ambapo Diwani wa kata ya Sanya juu Juma Jani alitaka kufahamu hatima ya wakulima baada ya mazao yao kuharibiwa Wanyama wakiwamo Tembo hasa kwenye mashamba ya Pongo na Leoni.

Diwani huyo Akizungumza kwenye Baraza hilo,ametaka kufahamu hatua zinafanyika kumsaidia wakulima ambao mazao yao yameharibiwa na Wanyama yakiwamo mahindi , maharage na alizeti

Jani amesema unakuta ya mwaka jana na hata ya mwaka huu mazao yanaendelea kuharibuka,nimetaka kujua ni hatua gani ambazo idara usika imezichukua kuhakikisha Wananchi wanalipwa fedha uharibifu wa mazao yao

Baada ya swali hilo Mwenyekiti wa halmshauri Dancan Urasa,alimtaka Afisa maliasili kutoa kujibu ya nini kinafanyika kunusuru mazao ya mkulima uko mashambani

Onesmo Haule kutoka idara ya maliasili katika majibu yake,amesma kwenye mashamba hayo kuna baadhi yanachangomoto ya umbali mpaka wa hifadhi ,ile kanuni imemaanisha mtu ambaye anastahiki kupata hiyo pole

Onesmo amesema shamba linapaswa kuwa walau umbali wa mita 500 kutoka kwenye mipaka au bikoni ya hifadhi,nitofauti kwa mkoa wetu hasa maeneo haya.

Kwa hiyo kimsingi tukienda kwenye kanuni inatutaka tupime umbali wa shamba lililopo au kwenye bikoni ya hifadhi,sasa pale ni tofauti hakuna hata mita 1 au mita 2 ,Kwa kweli katika maeneo haya ya mashamba ya Pongo ,Leoni na Lairongo yanachangomoto hiyo

Amesema hata hivyo kuna mpango ambao hawezi kuusema hapa mbele ya Bazara,siwezi kuweka bayana

Pia amesema kuwa wamekuwa na mpango mwingine ,tukasema maisha yenyewe ndiyo haya, Pongo ndiyo hivyo Leoni ndiyo hivyo,hatuwezi kuyaacha haya mashamba

“Ni kweli sasa tulionao mpango kwamba kuanzia msimu huu kuelekea msimu ujao tumetafuta wafadhili wa Shirika la kuhidhi Wanyama pori Duniani ambao watashirikiana nao kutoa elimu kwa Wananchi “amesema Onesmo

Amesema elimu hiyo ni kuwapa mbinu kukabiliana na Wanyama hao,Kwa sababu tumeshaona tukienda upande wa kifuta jasho ni changamoto sana

Kwenye malipo ni changamoto japo kuna utaratibu wanaoufanya kusaidia wale Wananchi wapate kifuta jasho

Awali Wilfred Urio mmoja ya wakulima hao amesema amekuwa akitumia muda mwingine kulinda mazao yasiharibiwe na Wanyama hao nakuacha shughuli zingine za kumuingizia kipato cha familia

Kwa upande wake Agustine Wiliadi anasema kila mwaka mazao yamekuwa yasiharibiwe na Wanyama,mwaka jana walifika Viongozi wa Serikali na kutuandika majina ili kutoa fidia lakini hawakurudi tena,hatukupata hiyo fidia

Mwisho