Site icon A24TV News

,Babu wa miaka (70),adaiwa kumlawiti mjukuu wake wa miaka( 8) Wilayani Hai

Na Bahati Hai,

Wananchi wa Kijiji cha Mashua kata ya Masama Magharibi Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro,wamelaani kitendo cha Mkazi wa Kijiji hicho Aliashiwanga Mmari (70),kudaiwa kulawiti mjukuu wake (8)Darasa la pili shule ya msingi Nsongoro

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mbaruku Mmari amesema ameshafikishwa kituo cha Polisi Bomang’ombe Wilayani humo

Wananchi hao wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti,wamesema kitendo alichofanya kwa mjukuu wake nicha kulaaniwa na kila mtu sasa na ,Sheria ichukua mkondo wake ili iwe fundishi kwa mambo haya yamekuwa yakiongezeka kila uchwao

“Ni kweli Sheria ichukue mkondo wake ,haya matukio yamekuwa yakijirudia rudia siku hadi siku juzi , tumeona kwenye mitaandao ya kijamii wale vijana wakimbaka msichana uko Dar esalam ,Serikali sasa sijui tunaelekea wapo”wamesema Wananchi hao

Madina Mollel Mmoja ya Wananchi hawa amesema Siku ya tukio alipigiwa simu na bibi wa huyo mjukuu akimtaka afike nyumba kwake

Anasema alipofika alimkuta akiwa na Mkuu wake na alimuekeza kuwa mtoto huyo amefanyiwa ukatili na Babu yake ,na aligundua hilo anapofua ngua za mjuku wake anakuta kinyesi

Madina amesema baada ya maelezo hayo walichukua hatua za kwenda hospital ya Wilaya ya Hai Kwa vipimo, ambapo ilibainika kwamba mtoto huyo ameharibiwa vibaya sehemu zake za haja kubwa

Nikitendo cha kinyama sana kama kweli Mzee huyo kama ameusika Sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundishi Kwa watu wenyetabia kama hizo ,haya mambo ya ukatili kila mara tunayasikia kwenye vyombo vya habari tumuombe Mungu atukinge na matukio haya

Hivyo Tunaomba taasisi zinazopinga vitendo hivyo wajitahidi kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari ili kunusuru watoto wetu na majanga kama haya,kinga ni bora ,tusisubiri

Ezikieli Mushi amesema hii imekuwa ni changamoto kubwa kwenye Kijijii hicho ,kwani sio mara ya kwanza shule hiyo ilishatokea tena baba mlezi kumlawiti mwanae wa Darasa la nne alikamatwa na kumpeleka mahakamani

Lakini cha kushangaza baada ya muda ameruidi nyumbani uraiani mpaka Leo mtoto anaishi katika nyumba salama

“Ni kweli mtoto yupo nyumba salama amehifadhuriwa ,lakini na baba mlezi yupo nyumbani anaendelea na maisha inatia uzuni”amesema Mushi

Aidha Mwenyekiti wa Kijiji hicho amesema taarifa hii aliipokea na kwamba mtuhumiwa alichukuliwa na jeshi la Polisi kituo cha Bomang’ombe,na kwamba mtoto baada ya vipimo vya hospital amerudi nyumba kwa bibi yake

Kamanda wa Police mkoani hapa Simon Maigwa,amethibitisha kukamatwa mtu huyo

“Ni kweli tunamshikilia mtu huyo kwa tuhuma za kufanyia ukatili mwanafunzi”amesema Maigwa

Mwisho