Site icon A24TV News

CHAMA CHA WAFANYAKAZI SERIKALINI TUGHE, IMEWATAKA WAJIRI KUWAPATIA SEMINA WATUMISHI WAKE

CHAMA Cha wafanyakazi wa Serikali,na afya (TUGHE) kimewaomba waajiri Nchini kuwapa haki wafanyakazi ya kujiunga na Vyama
vya wafanyakazi wanavyovitaka badala ya wao kuwachagulia Vyama hivyo.

Hayo yameelezwa Augosti 26 na Katibu mkuu wa Tughe ,Hery Mkunda,alipokuwa akifungua semina ya siku nne ya kuwajengea uelewa Viongozi wa matawi na waajiri kwenye Ukumbi wa Lushgadern na kusisitiza kwamba waajiri wasiwachagulie wafanyakazi Vyama vya kujiunga kwa kuwa kila mfanyakazi ana uhuru wa kujiunga na Chama akitakacho.

Amesema kila mfanyakazi ana haki ya kuchagua Chama cha kujiunga kulingana na Sekta anayotoka hivyo kumchagulia mfanyakazi Chama ni kwenda kinyume na utaratibu na sheria.

Amesema kuwa swala la mfanyakazi kujiunga na Chama chochote cha wafanyakazi ikiwemo Tughe, ni muhimu sana na ni haki ya mfanyakazi katika kulinda ,kutetea haki na masilahi ya wafanyakazi.

Amesema kuwa Vyama vya wafanyakazi havipo kwa ajili ya kutetea wafanyakazi waovu,wazembe, vitendo visivyofaa kwa watumishi ikiwemo uzembe ,Uvuvi,wizi,wala vitendo vyote vinavyoweza kupelekwa uvunjifu wa amani mahali pa kazi.

Amesema lengo la msingi la mafunzo hayo ni kujenga uelewa wa pamoja juu ya masuala ya ajira,na Utumishi kati ya waajiri na wafanyakazi na tayari matunda ya mafunzo hayo yameanza kuonekana ambapo migogoro kati ya waajiri na wafanyakazi imepungua kupitia njia ya majadiliano.

Amesema kwa muda wa miaka sita tangia mwaka 2018 Tughe imekuwa na utaratibu wa kuandaa na kuratibu mafunzo ya pamoja yanayojumuisha washiriki kutoka Viongozi wa matawi ya Chama hicho na mamlaka za ajira ambapo mwitikio umekuwa ukiongezeka .

Amewaomba wafanyakazi kutimiza wajibu wao kikamilifu wanapokuwa kazini akawakumbusha kwamba hakuna haki bila wajibu hivyo lazima watimize matakwa ya mwajiri sambamba na kufuata Sheria ,kanuni na taratibu zilizopo.

Mafunzo hayo yameshirikisha washiriki kutoka Wizara,Idara,Taasisi,Wakala wa Serikali,Bunge,Mahakama,Sekeretariet za mikoa,Mamlaka za Serikali za mitaa,Taasisi,za afya na Serikali na binafsi.