Site icon A24TV News

DCEA KANDA YA KASKAZINI YATOA ELIMU KINGA KATIKA KONGAMANO LA VIJANA NA WANAFUNZI WILAYANI MOSHI

Na Mwandishi wa A24tv .

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupam bana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 31.07.2024 kwa kushirikiana na Taasisi ya Tanzania Ex-Prisoners Foundation (TePF) imetoa elimu kinga juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya kwa vijana wa bodaboda, bajaji na machinga pamoja na wanafunzi kutoka Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCu) na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mwenge (MWECAU) katika Ukumbi wa CCM Mkoa uliopo wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Aidha, kauli Mbiu ya Kongamano hilo ilikuwa ni “_Ujana Bila Uhalifu, Inawezekana_”. Mgeni rasmi wa kongamano hilo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Zephania Sumaye kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu.

Pia, jumla ya vijana na wanafunzi 311 katika kongamano hilo walihimizwa kuachana na matumizi pamoja na biashara haramu ya dawa za kulevya ili waweze kutimiza ndoto zao.