Na Bahati Hai .
Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Amir Mkalipa ameipa kongole ,Taasisi ya Tanzania Islamic Teaching Association (TISTA), Wilayani hapo kupeana mawazo namna ya kufundisha elimu ya Dini Shuleni ,lakini pia namna ya kuona wanawasaidia watoto katika swala nzima la maadili na malezi ili waje kuwa raia wema wa Watanzania
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo wakati wa semina ya usimamizi wa mtihani wa Taifa wa EDK wa Darasa la saba iliyofanyika katika ukumbi wa Misikiti wa Safii Bomang’ombe Wilayani humo,na kuhudhuria na Walimu wa shule ya Msingi , Sekondari na Walimu wa Madrasa.
Mkalipa amewataka Walimu hao kuendelee kufundisha kujitoa kwa hali na Mali kufundisha watoto na kuwaandaa na kusome elimu ya Dini yao lakini na kufanye juhudi kubwa kusoma masomo mengine ili waweze kufaulu
Amesema lengo lao ni zuri Kwa sababu wanataka kuweka nguvu katika kuhakikisha watoto wanafanya vizuri masomo ya Dini na masomo mengine yote kuhakikisha watoto wanafaulu katika Wilaya hii
“Ni kweli niwaongeze taasisi hii na malengo yake ni mazuri ,niwatie moyo na kuwaunga mkono ,kwa sababu pia wanakusanya michango kwa ajili ya kuwasaidia kufanikisha watoto wasiojiweza kusoma shule mbali mbali ili ni jambo kubwa na la kupigiwa mfano na sisi tujitoa kama Serikali “amesema Mkalipa.
Wito wangu ni kuhakikisha mambo yote yanakwenda vizuri na kila mwenye uwezo wa kuchangia sehemu ili watoto wa kitanzania waweze kupiga hatua
Leo nimekuja kufunga kongamano ili la siku moja ,lakini pia mmezungumzia maadili katika kuitendea haki jamii inayowazunguka na watoto wenye mahitaji mkiwaandaa kimaadili ,kielimu ili waweze kuwa wanafunzi bora na raia wema niwapongenze sana
Nasibu sheikh wa Wilaya Masuud Mbowe,amesema vipindi vya Dini Shuleni vinasaidia sana watoto ,wananufaika na elimu
Amesema hata wale ambao kwenye Misikiti yao kwenye Madrasa zao hawakufanikiwa kupata elimu ,lakini wanapokuwa shuleni kikiwepo basi mafanikio ya kupata chochote katika maisha yake ya Uisilamu atakuwa amefanikiwa
Awali Hassani Marandu kutokaTaasisi hiyo mbali na kutoa elimu ya Dini shule pia wamekuwa wakiwafundisha mabadili mema wanafunzi na namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili ikiwamo kubakwa na ulawiti
Mwisho