Site icon A24TV News

HALMASHAURI YA SIHA YAPEWA KONGOLE KWA KUA KINARA KATIKA MIRADI

Na Bahati Siha
Halmshauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro,imepewa kongole kwa kufanya vizuri katika vigezo vitatu Vigezo hivyo ni ujenzi wa Miradi mbali mbali ya maendeleao Kwa kufikia asilimia 95,uchumi wa halmshauri unaenda vizuri,na kigezo kingine ni kupata hati safi miaka mitatu mfululizo

Ponceano Kilumbi kutoka ofisi ya katibu tawala wa mkoa huu ,akizungumza katika kikao cha Baraza la maalumu la mwaka kupitia shughuli zote za halmshauri katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024, katika ukumbi wa halmshauri hiyo,amesema halmshauri hiyo inafanya vizuri sana nakuonye wasirudi nyumba kuwaletea maendeleao Wananchi wa Siha

“Ni kweli nasema Siha wanakwenda vizuri utokana na vigezo ambavyo vinaonekana vya kuonyesha kwamba Siha unakwenda vizuri “anesema Kilumbi

Kilumbi amesema yeye kama mwakilishi wa katibu tawala wa mkoa anavyo vigezo vya kuonyesha Siha unakwenda vizuri ukilinganisha na uchumi wa mwaka juzi na mwaka Janani tofauti

Siha hii mwaka wa fedha uliopita ilikuwa a asilimia 126 ya mapato yake ya halmshauri na Kwa maana hiyo basi katika mkoa wa Kilimanjaro hii ndiyo Wilaya pekee ambayo imefanya vizuri sana kwenye mapato ili sio jambo ndogo

Amesema kigezo cha pili amesema wao kama Serikali uwa wanafutilia Serikali inapoleta hela kwenye taasisi kama hii ya halmshauri,lakini vilevile hela halmshauri inayokusanya mapato mapato hayo inayokusanya ni pesa ya umma.

Kwa hiyo pesa inayoletwa na Serikali kuu na pesa inayokusanywa na halmshauri lazima itumike kulingana na Sheria na kanuni za fedha kwenda kinyume na utaratibu huo ni kutafusiriwa pesa kutumika kwa malengo yasiyokusudiwa

Siha wanakwenda vizuri,kwanza wamepata hati safi zaidi ya miaka mitatu mfululizo ,lakini vilevile pamoja na kupata hati safi,wamefanya vizuri sana katika kujibu hoja ambazo zilikuwa zimetolewa na Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali ( CAG), ambapo walikuwa na hoja 25 katika hoja 25 wameweza kujibu 19 na hoja hizo zikafungwa

Amefafanua Kwa kusema kwamba i jambo kubwa ni uwazi kwamba menejement inafanya kazi vizuri ,pesa ya Serikali ambayo inaletwa na pesa ya kwa maana ya maana ya halmshauri inayokusanywa inaingia kwenye kapu la Serikali na inatumika kulingana na sheria na kanuni

Aidha amesema jambo la tatu ni swala la Miradi ,Miradi ya maendeleao ya wilaya ya siha ukifika kwa asilimia 95 miradi ya maendeleao ipo vizuri ukikagua thamani ya fedha inaonekana

Kwa hiyo niwapongenze Kwa vigezo hivyo vitatu kwamba mnakwenda vizuri ,endeleeni hivyo msirudi nyuma, msibweteje ili Wananchi wa Siha wafaidi matunda ya kazi.

Juma Jani Diwani wa kata ya Sanya juu,amesema wao kama madiwani Kwa dhati kabisa wanajisikia wamoja wanajisikia kutimiza wajibu wao kama madiwani Kwa kushirikiana na wataaluma wa halmshauri

Mwenyekiti wa halmshauri Dancan Urasa niwapongeze Madiwani, Mkurungenzi mtendaji wa halmshaurina timu yake,Mbunge wa Jimbo hilo CCM pamoja na ofisi ya mkuu wa wilaya kwa ushirikiano wao ndiyo tumefikia hapo ,na kuomba ushirikiano huo uendelee

Mwisho