Site icon A24TV News

Halmshauri ya Hai yapewa kongole Kwa ujenzi wa Miradi iliyo bora na thamani ya fedha ikionekana

Na Bahati .Hai

Halmshauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro,imepewa kongole kwa matumizi ya mazuri ya fedha zilizotolewa na Serikali katika ujenzi wa Miradi mbali mbali ya maendeleao ikiwamo vyumba vya madarasa ,vituo vya Afya pamoja na barabara

Haya yamesemwa na Gasp Ijiko kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa katika Baraza maalumu Kwa ajili ya kupitia shughuli zote za halmshauri katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024,

Akizungumza katika Baraza hilo liliofanyika katika ukumbi wa halmshauri hiyo, amesema halmshauri hiyo ni miongoni mwa halmshauri zilifanya vizuri kwenye ujenzi wa miradi

“Ni kweli mfano eneo la Elimu Msingi eneo la Sekondari na ushirika kote kumeonyesha kwamba fedha hizi zimetumika katika ujenzi wa miundombinu

Tumepata kipengele kizuri sana kinachoonyesha miundombinu ambayo imejengwa katika Kila idara mahususi na hii imedhihirisha kwamba fedha hizi ambazo zimetolewa halmshauri ya Wilaya hii zimetendewa haki

Na Miradi inaonekana na ndiyo maana katika halmshauri zenye Miradi mizuri ni pamoja na halmshauri hii,Kwa hiyo fedha mmezitendea hakinendene mkazitangaze

Fedha nyingi kutoka Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhuu Hassani,Miradi mkaitangaze bila uoga watu waone watu wafahamu, Mwenyekiti nikupongeze taarifa yako kutoka ukurass wa kwanza mpaka wa mwisho ni zuri,endeleeni na mshikamano

Awali Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Edmund Rutaraka,akisoma taarifa yake,amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023, halmshauri imefanikiwa kutekeleza shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii

Amesema kila sekta Kwa lengo la kutoa na kuinua ubora kwa huduma Kwa Wananchi,vilevyotekelezwa ni pamoja na utawala bora , Sheria,mawasiliano,teknolojia ya habari,elimu,Afya, Ustawi wa jamii, kilimo, mifugo,uvuvi,Aridhi,na uwezeshwaji Wananchi kiuchumi

Juhudi hizi zimetekelezwea na halmshauri kushirikiana na Serikali kuu,ofisi ya mkuu wa mkoa, CCM,mkuu wa Wilaya pamoja na wadau wa maendeleao,tunamshukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhuu Hassani imewezesha mafanikio yote

taarifa Mwenyekiti wa (UWT )Wilaya hiyo Happynes Eliufoo,amesema hayo yote ni kutokana na mausiano mazuri kati ya CCM na madiwani , Watendaji,pamoja na wataalamu hivyo tuendeleo kudumisha mausiano

Mwisho