Site icon A24TV News

Jela Miaka 30 kwa kosa la kulawiti mtoto wa kaka yake umri wa miaka( 19)

Na Bahati Siha,

Mkazi wa Kijiji cha Merali Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro Kanti Mbuya (45),Mkulima amehukumiwa kwenda kutumikia kifungo cha Miaka 30 jela kwa kosa na kulawiti mtoto kaka yake mwenye umri wa miaka (19 )

Mwendesha mashitaka wa Serikali David Chisimba mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi mwandamizi wa Mahakama hiyo Jasmine Abdul, amesema kwamba tukio hilo limetokea March 10 mwaka huu,na kijana huyo alikuwa akiishi kwa bibi yake

Mwendesha mashitaka huyo ameeleza kuwa mshitakiwa siku ya tukio alimfuta kijana huyo kwa bibi yake na kumchukua lengo la kumpa shughuli flani

Baada ya kufika nyumbani mshitakiwa alimuita chumbani na kutishia ambapo alianza kumuingilia kinyume na maumbile kuanzia March 10 hadi march 14 mwaka huu.

Muhanga aliporudi nyumbani Bibi yake alimuona katika hali isiyoyakawaida,ndipo alipowaita Uongozi wa Kijiji nakueleza tukio zima

Kosa hilo ni kinyume na kifungu 154(1)(a)na( 2) kilichofanyiwa marejeo 2022,,kesi hiyo ilikuwa na mashahidi 5 akiwamo Muhanga mwenyewe ,Bibi pamoja na Daktar

Kabla ya kutolewa kwa hukumu mshakiwa alitakiwa kujitetea ,ambapo amesema Kwa sababu ni kosa lake la kwanza Mahakama imuonee huruma

Hata hivyo kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hivyo Mahakama inakuhukumu kwenda jela kutumikia kifungo cha maisha 30 jela

“Ni kweli vitendo vya ubakaji na ulawiti vinazidi kuongeza ndani ya Wilaya yetu ili iwefundisho kwa wengine unakwenda kutumikia kifungo cha Miaka 30 jela”amesema Jasmin,kesi hiyo namba CC 8088/2024

Mwisho