Site icon A24TV News

KATIBU TAWALA WA MKOA WA KILIMANJARO ATOA ONYO KWA WATUMISHI UPOTEVU WA FEDHA ZA UMMA

Na Bahati Hai.

Katibu tawala mkoani Kilimanjaro,Kiseo Nzowa amewataka Watumishi wa Halmshauri ya Hai mkoani hapo,kuzuia mienya ya upovu wa mapato yanayokunywa na Halmshauri hiyo

Amesema katika eneo moja linyeshida sana Serikalini ni hilo,wanakusanya wanatia katika kapu ambalo lina matobo,

Akizungumza katika kikao cha kawaida cha Bazara la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmshauri hiyo,amesema katika eneo hilo linachangamoto sana hivyo liangaliwe sana

” tujitahidi sana kuzuia mianya ya upotevu wa mapato kama nilivyosema katika eneo hili linashida sana Serikalini sababu mnakusanya mnatia katika kapu lililo na matobo kuna mchwa ambao wanatafuna hapana hii haikubaliki”amesema Nzowa.

 

Nzowa amesema kutokana na kuwa na changamoto hiyo ni vizuri kuhakikisha kwamba wanazuia upotevu wa aina yeyote hile ,na katika hili lazima wawe wakali kuhakikisha Kila kinachukusanywa kinakusanywa kwa ukamilifu wake

Lakini pia kinatumika kufuata utaratibu unautakiwa ,Kwa hiyo tujitahidi sana kuzuia upotevu huo

Hata hivyo ameipongeza halmshauri hiyo Kwa kukusanya mapato na kufikia zaidi ya asilimia 100 ,ni jambo la kujivunia.

Wito wangu kuwa isiwe hadhithi ya mgema,akisifiwa analitia maji mnarudi nyuma ,niwaomba sana muendelee na spriti hiyo ,yale malengo ya ukusanyaji mapato ili Miradi mbali mbali iweze kukamilika mliyoianzisha

Mkungenzi mtendaji wa halmshauri hiyo Dionis Myinga,amesema ushirikiano uliopo katika ya Watumishi na Madiwani pamoja na mkuu wa Wilaya hiyo Amir Mkalipa ndiyo sababu yakufikia ukusanyaji huo wa mzuri wa mapato ya halmshauri.

Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Edmund Rutaraka,amesema maelekezo yaliyotolewa wanaamini na watakwenda kusimamia vema na kuhakikisha wanafikia malengo ya halmshauri.

Mwisho