Site icon A24TV News

MAIPAC yazindua elimu ya mpiga kura yataka vijana kujiandikisha

Mwandishi wetu. Arusha.

Taasisi ya Waandishi wa habari ya MAIPAC jana imezindua mradi wa utoaji elimu ya mpiga kura kwa mkoa Arusha na kuwataka vijana waliofikisha miaka 18 wenye sifa , kwenda kujiandikisha katika daftari la Kudumu la wapiga kura.

Wakizungumza katika uzinduzi wa utoaji elimu ya mpiga kura, Mkurugenzi wa MAIPAC,Mussa Juma na Meneja miradi wa Taasisi hiyo,Andrea Ngobole katika kituo cha Radio Sunrise Fm Arusha,walitaka vijana kuanza kujiandaa sasa kujiandikisha katika daftari la Kudumu la wapiga kura.

Juma alisema vijana wenye umri kuanzia miaka 18 wanasifa ya kujiandikisha katika daftari Hilo kama hawajapoteza sifa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi au sheria nyingine zilizotungwa na bunge.

“Vijana mara nyingi wamekuwa wakishiriki katika mikutano ya kisiasa lakini hawajitokezi kujiandikisha kupiga kura na wele waliojiandikisha baadhi Yao wamepoteza vitambulisho Sasa hii ni fursa nyingine kupata haki Yao”alisema

 

Hata hivyo juma alisema zoezi likianza na kuboresha daftari mkoa Arusha,wanaotaka kujiandikisha au kuboresha taarifa zao haipaswi kutoa taarifa za uongo, kujiandikisha zaidi ya mara Moja.

“Lakini pia kuna Tabia ya kuuza ama kununua kadi ya mpiga kura jambo hili halipaswi kufanyika au pia hata kuharibu kadi ya mpiga kura”alisema

Kwa upande wake Ngobole alisema tume huru ya uchaguzi imeandaa vituo vya kutosha vya kujiandikisha au kuboresha taarifa hivyo ni muhimu kujitokeza.

“Vituo vya kujiandikisha ambavyo tayari vimetangazwa vitafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa 12 jioni hivyo tujitokeze”alisema

Taasisi ya MAIPAC ni miongoni mwa Taasisi ambazo zimepitishwa na tume huru ya Uchaguzi kutoa elimu ya mpiga kura mwaka Hadi mwezi Machi mwakani.

Mwisho.