Site icon A24TV News

MWENYEKITI WA HALMASHARI YA SIHA, AMVAA MKURUGENZI KWA UTUNZAJI MBAYA WA MAZINGIRA

Na Bahati Siha

,Mwenyekiti wa halmshauri ya Siha mkoani Kilimanjaro Dancan Urasa amehudhunishwa na ukataji miti hovyo Wilayani humo jambo ambalo linakwenda kinyume na juhudi za Rais Samia Suluhuu Hassani la utunzaji wa mazingira

Hivyo kumtaka Mkurungenzi mtendaji wa halmshauri Haji Mnasi kuwaagiza watendaji wa vijiji na kata wasimamie Sheria katika Maeneo yao ili mazingira yabaki salama.

Akizungumza katika kikao cha kawaida cha Baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmshauri,amewataka Mkurungenzi kutoa maagizo kwa watendaji hao kusimamia zoezi hilo ili kunusuru Siha kuwa jangwa

“Ni kweli nimetoa nimeagiza kupitia Kwa Mkurungenzi mtendaji wa halmshauri hii,kuwaagiza watendaji wa vijiji na kata katika Maeneo yao kusimamia Sheria Kwa kuchukua hatua ,tukisema tukae kimiya wata maliza miti yote”amesema Dancan

Dancan amesema ukipita Maeneo mengi unaona miti imekatwa ,sasa hatuwezi kukaa kimya kwa watu wanaoharibu mazingira katika Maeneo yetu ,lazima tumuunge mkono Rais Samia Suluhuu Hassani katika kupambana na dhidi ya waharibifu hao wa mazingiratunzaji wa mazingira ili Wilaya yetu ibaki ya kijani

Hivyo nimemuomba Mkurungenzi mtendaji kupitia Kwa watendaji hao kusimamia Sheria miti isikatwa hivyo na zoezi la upandaji miti likithiri kwa wingi

Baadhi ya Wananchi wameipongeza taarifa hiyo ya Mwenyekiti akiwamo Mahamedi Mzava kuhusu swala la mazingira, sasa limekuwa janga la kitaifa kwa sababu watu hawatunzi mazingira.

Mzava amesema hapa Siha watu wa kitengo cha mazingira wanausika kwa kiasi kikubwa kutoa vibali vya kukata miti bila kuhakiki,miti inakatwa kwa sababu gani

Amesema wao wakiwa umri wa kati ulikuwa ukikaa kule nyumbani sehemu za mlimani i hauoni nyumba kutokana na miti kuwa mingi wazee waliona umuhimu wa kutunza mazingira ,lakini kwa sasa miti inakatwa tuu ,tunaomba wale walizopewa jukumu la kutunza mazingira wasimame Kwa haki

Mbali na hilo la mazingira ampongeze Mkurungenzi mtendaji na timu yake kwa ukusanyaji wa mapato na kufikia asilimia zaidi ya 100,ambapo amesema ni jambo la kheir ,kwani shughuli za halmshauri haziwezi kwenda bila ya kuwa na mapato

Nkin Diwani wa kata ya Livishi amesema ushirikiano huo mzuri kati ya Madiwani na Watumishi pamoja na ofisi ya mkuu wa Wilaya ndiyo imesababisha kufikia asilimia hizo,hivyo kuomba ushirikiano huo kuendelea

Ambapo pia amempongeza Rais Samia Suluhuu Hassani Kwa kutumia fedha nyingi Kwa Miradi ya maendeleao Wilaya humo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule vyumba vya madarasa,mabweni vituo vya Afya pamoja na barabara

Mwisho