Site icon A24TV News

Mwenyekiti wa Kamati ya chakula agoma kujiudhulu nafasi yake licha ya kutakiwa kufanya hivyo na Wazazi Siha

Na Bahati Siha .

Wazazi na walezi wa shule ya Sekondari Naisinyar kata ya Orkolili Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,wamemtaka Mwenyekiti wa kamati ya chakula wa shule hiyo Daniel Nnko kutekeleza azimio la mkutano wa wazazi likimtaka kujiudhulu mara moja

Hii ni kutokana kutumia madaraka vibaya ikiwa ni pamoja nakutokusoma mapato na matumizi ndani takribani miaka 9 kitu ambacho kinachangia kurudisha maendeleao nyuma ya shule hiyo,nakumuomba mkuu wa wilaya Christopher Timbuka kufika shuleni hao.

Wananchi hao wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti,wamemtaka Mwenyekiti huyo kutekeleza azimio hilo kabla hatua nyingine za kinizamu hazijachukuliwa dhidi yake

“Ni kweli kwenye kikao hicho tulimpa muda wa kujiondoa kwenye madaraka ili nafasi apewe mtu mwingine ,lakini tunashangaa amekomaa yupo mtaani akikusanya fedha kwa wananchi bila hata kushirikisha Viongozi wa vitongoji “wamesema.

Ernest Lymo mkazi wa Orkolili mmoja ya wazazi hao ,amesema wazazi walifika maamuzi hayo kutokana kutokuwa na Imani na matumizi ya fedha zao wanazotoa kwa ajili ya michango ya shule kutokusomewa mapato na matumizi takribani miaka 9 pia kuendesha mambo yake kwa ubabe

Sasa kutokana na Mwenyekiti kukaidi maazimio ya mkutano huo wa wazazi ,kinaonyesha kwamba hayupo pekiyake,wapo wanaomuinga mkono ili aindeleze mamba yake ambayo hayana tija katika shule yetu ndiyo maana tunamtaka Dc,Timbuka afike hapa shuleni

Ernest amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 600 na kila mzazi anachangia sh,laki moja na sabini na tano kwa mwaka hii ni fedha nyingi hataki upeleke mahindi kama chakula anataka fedha thasilimu.

Elisante Nasar Mwenyekiti wa kitongoji makao mapya amesema Matatizo tunayopata hapa orkolili yamekuwa kero kwa Wananchi, Mwenyekiti huyo ,yeye ni Mwenyekiti wa kamati ya chakula,yeye ni makamu Mwenyekiti wa bodi ya shule na pia ni Mwenyekiti wa CCM kata hii ya Orkolili

Emanuel Nasar mkazi wa kitongoji cha Makao mapya ameomba chama na Serikali itasaidia kuangalia swala hili ,ikiwezekana waje wakaguzi kuja kukagua hii shule kulingana na fedha tunazochanga tuone zinavyotumika , kifanyike kikao cha wazazi na pia tunamuomba Munge awepo siku hiyo

Daniel Nnko ambaye ndiyo Mwenyekiti wa kamati ya chakula akizungumza swala hili,kwanza alikanusha kuwe yeye sio Mwenyekiti wa kamati hiyo,yeye ni mjumbe na kwamba Mwenyekiti wa kamati anaitwa Steven Mtulwa

Amesema wameshasoma mapato na matumizi junuar na June mwaka huu na wana kibali kutoka kwa mtendaji kuendelea na ubambuzi Kwa lengo la watoto kupata chakula Shuleni,kinachoendelea ni maswala ya siasa

Mtendaji wa kata hiyo Bertord Mtolera amesema kuwa Kuna makundi mawili ,kuna linataka atoke na kingine linataka abaki,kwa hiyo kuna makundi mawili yanakidhana hii ndiyo changamoto
,

Mwisho