Site icon A24TV News

SENDIGA AFUNGA MAONESHO YA NANE NANE ARUSHA IAA YAIBUKA KIDEDEA YABEBA KOMBE

Juma Tano ya tarehe 8 Mwezi wa 8 2024 .

Na Geofrey Stephen Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya NaneNane na sherehe za wakulima mwaka 2024 kwenye viwanja vya Nanenane Themi -Njiro mkoa wa Arusha mapema leo Agosti 08,2024.

Kauli Mbiu: ” Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”

Katika Maonesho hayo Chuo Cha Uhasibu Arusha IAA imeibuka kidedea mara baada ya kupata  kombe wakiwa washindi wa Pili katika  kundi la Taasisi za Elimu na Mafunzo katika Maonesho ya NaneNane Kanda ya Kaskazini yaliyofungwa leo rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga katika Viwanja vya Themi, Njiro Jijini Arusha.

Sendiga akitoa tunzo hizo amepongeza Aiaa kwa kuendelea kutoa elimu iliyo bora na kuendeleza kupata vikombe vya kufanya vizuri kama miaka mingine jambo ambalo linavutia wanafunzi na watumishi kujiunga na chuo hicho katika kozi mbali mbali chuoni hapo .

MERU DC KINARA MKULIMA NA MFUGAJI BORA KANDA YA KASKAZINI.

Halmashauri ya Wilaya ya Meru, imeshika nafasi Ya kwanza Mkulima na Mfugaji hodari kufuatia mashindano ya Maonesho ya NaneNane na sherehe za Wakulima Kanda ya Kaskazini.

Mkulima Penina Ndelekwa Nnko kutoka halamshaurinya Meru wilaya ya Arumeru ameibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza kwa mikoa yote mitatu ya Kanda ya Kaskazini Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

Mwisho .