Site icon A24TV News

Simba Tawi la Hai wafanya jambo nzuri Kwa kukumbuka yatima mujibu wa vitatu vitakatifu Quran na Bibilia

Na Bahati Hai,

Jamii imetakiwa kuwathamini watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuwapa mahitaji muhimu kama elimu,maladhi,chakula na mavazi ili waweze kutimiza ndoto zao.

Haya yamesemwa leo na Ramadani Shabani katibu wa Simba Tawi Bomang’ombe Wilaya Hai mkoani Kilimanjaro,wakati wa maadhimisho ya siku ya Simba,ambapo waletembelea kituo cha watoto yatima Kao la Amani Bomang’ombe Wilayani hapa na kutoa msaada ikiwa pamoja na Mchele,sabuni pamoja na mafuta ya kupikia.

Akizungumza Mara baada ya kukabidhi vitu hivyo,ameitaka jamii kuthamini watoto hao ili kuwapunguzia mawazo ya kuwafikiria wazaza wao ,hata vitabu vitakatifu Quran na Bibilia ina himiza jambo hilo

“Ni kweli vitabu vitakatibu ikiwamo Quran na Bibilia inaimiza sana watu kuwajali watoto hao,hata sisi siku ya Leo ya Simba tumeona tusherekee Kwa kufika katika kituo hiki”amesema Ramadhani.

Ramadani amesema watoto yatima wanastahili kupata haki zao za msingi kama vile ilivyo kwa wengine,kwani kufanya hivyo inawapunguzia mawazo ya kuwawazia wazazi wao

Kikubwa ni kukumbushana kuwathamini watoto hao kama vile tunavyowathamini watoto wetu ,kwani hakuna aliyeomba uyatima unakuja wenyewe

Kwa upande wake Monica Tukay kutoka kituo hicho,amewapa kongole wapenzi hao wa Simba Kwa kufika katika makao hayo na kutoa misaada hiyo.

Ambapo amesema katika kituo hicho wanalea makundi ya aina tatu , kwanza ni wtoto ambaye ametelekezwa na jamii aidha Baba na mama wamefariki yule mtoto amebaki hana malezi maalumu labda ameachiwa bibi,sasa Bibi hana uwezo wa kumlea huyo mtoto

Monica amesema kundi la pili ni watoto wanaofanyiwa ukatili ikiwamo kubakwa na kulawitiwa ile kesi inapoendeshwe kula mahakamani yule mtoto anapelekwa sehemu salama zaidi ambapo ni makao kama haya.

Ile kesi inaweza kuchukua muda wa mwaka mmoja au miwili mpaka wanapojiridhisha yule mtoto anarudishwa tena kwenye jamii

Kundi la tatu kabisa ni wale watoto wanaookotwa masokoni njiani aidha ametelekezwa au amepotea ndugu zake wanamtafuta,anakuwa yupo makao hayo

Amesema kituo hicho wanakiendesha misaada kutoka Serikalini na wasamaria wema wenyemapenzi mema kama walivyokuja watu wa Simba,hivyo kuomba wadau mbali mbali kujitokeza kuwaunga mkono

Mwisho