Site icon A24TV News

TEMBO WAVAMIA MASHAMBA YA WAKULIMA SIHA WAKULIMA WALIA NA SERIKALI KUHUSU TEMBO

Bahati Siha,

Wakulima wa mashamba ya Pongo,leoni na Molomo Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,wamesema wamekuwa wakipoteza muda mwingi kulinda mazao yaliyopo shambani yakiwamo mahindi,maharage na alizeti yasiharibiwe na Wanyama akiwamo Tembo

Kutokana na jambo hilo wameomba Serikali kufanya utafiti wa kina wa namna ya kuzuia Wanyama hao wasiendelee kuharibi mazao ya wakulima hao na kufanya kupata hasara na pia familia kukosa chakula.

Wakiongea na waandishi wa habari walipotembelea mashamba hayo na kuona jinsi yalivyoharibiwa Wananchi hao ,wamesema kwa sasa wamehamia mashamba na kupiga kambi mpaka watakapovuna

Wilfred Urio kutoka Kijiji cha Mowo njamu,amesema kwa sasa aneacha shughuli nyingine za kumuingizia kipato anafanya kazi ya kulinda chakula cha familia yake.

Amesema toka apande mahindi katika shamba hilo mpaka kuvuna yeye yupo hapo kwa muda wa miezi 6 akilinda mahindi ili kupata chakula cha familia

Kwa mfano amesema shamba lake akilima na kupanda analinda Nyani asifukue mahindi ,hapo hapo yanafikia hatua ya kuchanua Tembo na Mbogo wanakuja,kwa hiyo hapa tunalinda Wanyama wa aina tatu ,mpaka kuvuna huyapeleke nyumbani ndiyo utoke hapo hapa ni sawa na mateso

Hivyo tunaomba Serikali ituangalizie namna tuu ya utafiti ili kuona kwamba wanaweza kuzuia Wanyama waharibifu ,tunatumia muda mwingine kulinda mazao hayo ,tunaacha kufanya shughuli nyingine za kuleta maendeleao

Abdul Issa gharama ni kubwa kukaa uku kulinda mazao ,gharama kubwa kutunza mazao haya ,hatuna mbinu ya kuzuia Hawa wanyama zaidi ya kupiga kelele wakati mwingine ni kuhatarisha maisha,tunaomba Serikali ituletee baruti au wabuni kitu ambacho kitaweza kuwafukuza

“Ni kweli kutunza mazao ni gharama kubwa ikiwa ni pamoja na muda ,muda ambao ulikuwa ufanye shughuli zingine za kinaendelea,hapo bado haujafika sokoni ukakutana na ujazo wa rumbesa wa wafanyabiashara kwa kweli mkulima anashida sana Ila basi tuu”akiongea kwa masikitiko Abdul.

 

Agustine Wiliadi , anasema kila mwaka wanakumbana na kadhia hiyo,mwaka jana walikuja Viongozi wa Serikali kufanya tathimini na wakatuandika majina ili kutoa fidia lakini hawakurudi tena ,hakuna fidia yeyote ikitolewa

Onesmo Haule kutoka ofisi ya maliasili Wilayani humo,amesema taarifa wanazo kuhusu Wanyama hao na kwamba juhudi zipo zinafanyika

Mwisho