Site icon A24TV News

TIGO YAZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI YA HAKUNA MATATA KWA HAJILI YA WATALII

Na Grofrey Stephen Arusha .

Kampuni bora ya Mawasiliano nchini Tigo  imezindua kampeni ya hakuna matata kanda ya  kaskazini ikiwa na lengo kubwa kwa matumizi ya watalii wanaofika kutembelea mbuga mbali mbali.

Mapema leo jijini Arusha Akizindua kampeni hiyo Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini  Henry Kinabo amesema wanashukuru kwa  hatua nyingine kubwa na muhimu katika safari yao ya  kuboresha huduma za mawasiliano na teknolojia kwa ajili ya sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo sekta ya utali.

Mkutugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Henry Kinabo Akiongea na Vyombo vya Habari juu ya kampeni hiyo

Amesema Tunajivunia kuwa mbele ya vyombo vya habari kufanya uzinduzi na kutangaza kwamba  uzinduzi wa kampeni ya ‘Hakuna Matata hapa Arusha ikiwakilisha Kanda yote ya Kaskazini, baada ya mafanikio makubwa waliyo yapata  huko Zanzibar ambapo walizindua kampeni hiyo mwezi uliopita July 2024 .

Ameeleza kwamba Kampeni hii imelenga kuboresha uzoefu wa watalii wa kimataifa kwa kuhakikisha kuwa wanapata mawasiliano ya uhakika na kwa urahisi ili waweze kufurahia vivutio vya Utalii,

“Katika dunia ya leo, mawasiliano ni muhimu sana. Watalii wanaotembelea nchi yetu wanahitaji kuwa na mawasiliano bora, si tu kwa ajili ya kujuliana hali na wapendwa wao bali pia kwa ajili ya kupata taarifa muhimu na kuendesha shughuli zao kwa urahisi. Hivyo basi, kupitia kampeni ya ‘Hakuna Matata’, tunawaletea vifurushi maalum vya Jambo Packs’, ambavyo vitawapa watali i huduma bora na rahisi za mawasiliano” Alisema kinabo .

Watalii wakifuraiya uzinduzi wa huduma ya hakuna matata .

Matunaamini katika ubunifu na ubora wa huduma zao ni kwamba wamewekeza sana katika kuboresha miundombinu ya mawasiliano ikiwemo kusambaza teknolojia ya 4G kila kona ya Tanzania Pamoja na 5G yenye kasi zaidi kwenye miji ya kimkakati.

Uwekezaji huu utahakikisha kuwa watalii  wanapata huduma bora za mawasiliano kila wanapokuwa katika vivutio vyetu.

Kampeni hii ni sehemu ya mkakati wa kuboresha sekta ya utali ambayo ni sekta muhimu sana kwenye uchumi wa kanda hii ya kaskazini na taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi kinabo amesema ili watalii waweze kufurahia kampeni hii ya Hakuna Matata watafanya usajili wa e-SIM au kununua laini zao za Tigo  katika maeneo yao iwe hotelini au katika migahawa ambapo watakuwa na watoa huduma kwa Watalii wakishasajiliwa wataweza kufurahia Jambo Packs kwa kupiga *147*00# ambapo wanapata vifurushi mahususi kwa ajili yao.

Mwisho .