Site icon A24TV News

ASKOFU DKT. SOLOMON MASSANGWA ASTAAFU KWA HESHIMA KATIKA KANISA LA KKKT KIMANDOLU WAUMINI WAMLILIA, MACHOZI YA FURAHA

⁸Na Geofrey Stephen

Baba Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania – Dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt. Solomon Jacob Massangwa amestaafishwa kwa heshima, baada ya kuhudumu katika Kanisani hilo kwa miaka 42.

Ibaada maalum ya kumstaafisha Askofu Dkt Massangwa imefanyika kanisa la KKT Usharika wa Kimandolu, Jumapili ya leo Septemba 29, 2024 Jijini Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameshiriki ibada hiyo huku Usharika wa Kimandolu Mkoani Arusha ukimshukuru na kumtaja Askofu Solomon kwa kuhamasisha kulipa madeni ya kanisa, Kuongeza fursa za elimu kwa wachungaji wapya, Kuboresha ibada kwa Kuongeza wataalamu wa Muziki kwenye Dayosisi na kuongeza uinjilishaji kwenye majimbo ya Maasai kusini na Kaskazini

RAIS SAMIA ATOA MILIONI 20 KWA BABA ASKOFU MASSANGWA KWA KUWA KINARA WA AMANI YA ARUSHA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumapili Septemba 29, 2024, ametoa jumla ya Shilingi Milioni 20 kwa Baba Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, ambaye amestaafishwa rasmi hii leo kwa heshima na kanisa hilo mara baada ya kumaliza muda wake wa utumishi wa miaka zaidi ya 42 ndani ya Kanisa hilo.

Kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda aliyehudhuria ibada hiyo iliyofanyika Kwenye Kanisa la KKKT Usharika wa Kimandolu Jijini Arusha, Mhe. Makonda amemtaja Baba Askofu Dkt. Solomon Massangwa kama miongoni mwa nguzo muhimu zilizosaidia katika ukuzaji na utunzaji wa amani ya Mkoa wa Arusha.

“Baba Askofu Massangwa ni miongoni mwa Maaskofu waliojenga Amani, umoja na mshikamano katika Mkoa wetu wa Arusha, Hata kwenye nyakati ngumu ambazo serikali zilipita, Baba Askofu alibaki kuwa na utiifu na uaminifu ya kwamba Mungu atafanya. Alama zako tutazitunza nami nitakuwa sehemu ya kuhakikisha kwamba kila pando jema ulilopanda linaendelea kukua na kuendelea kuwa na matunda mema kwaajili ya mkoa wetu.” Amesema Mhe. Makonda.

Aidha Mhe. Makonda katika salamu zake kwa waumini wa kanisa hilo amewakumbusha na kuwasisitiza waumini wa dini ya Kikristo umuhimu wa kuwatunza na kuwalea Viongozi wastaafu wa Kanisa hilo akisema ipo tabia ambayo ni chukizo kwa Mwenyenzi Mungu ya Makanisa na waumini wa dini hiyo kuwasahau Viongozi wao Pindi wanapostaafu.