Site icon A24TV News

BAKWATA Siha waandaa mpango mkakati wa kushiriki mashindano ya Quraan Kimataifa

Na Bahati Siha .

Baraza la Waislmu Tanzania (BAKWATA),Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro,limesema litaanza kuwapiga msasa Walimu wote wa Madrasa Wilayani humo namna bora ya usomaji Quraan Tukufu ili kuwe na tija kwa wanafunzi na kushiriki mashindano ya kimataifa

Haya yamesemwa leo na Sheikh wa Wilaya hiyo Abubakar Hashimu, katika kikao maalumu kwa ajili ya kutathimini mashindano ya usomaji Quraan yaliyofanyika uwanja wa Benjamin Mkalipa Dar es salam hivi karibuni , ambapo baadhi ya Waumini kutoka Mkoa wa Kilimanjaro walifika katika tukio hilo.

 

Akizungumza na Waumini mbali mbali waliofika kwenye kikao hicho kilichofanyika eneo la Msikiti wa SanyaJuu ambapo ,masheik wa kata,Walimu wa Madrasa pamoja na Maimamu wa Misikiti , amesema ili kupata wanafunzi bora , lazima wakae na Walimu wa madrasa kwa pamoja

“Ni kweli kwenye kikao hiki ,tumekubaliana kwamba tutakaa na Walimu wa Madrasa,tutafanya nao vikao mbalibali,laki pia ili kufikia lengo la watoto kusoma vizuri na kuingia kwenye mashindano ya Kitaifa na Kimataifa ,lazima tuwe na mkakati”amesema. Sheikh Abubakar

Abubakar amefafanua zaidi kwamba baada ya kutoka kwenye mashindano hayo,walihamasika na wao kama Wilaya kushiriki ,lakini kushiriki uko lazima kuwe na maandalizi.

Sasa maandalizi lazima tukae na Walimu hao ,kusoma ukikosea neno moja linaweza kuleta maana nyingine tumeamua kukaa kwa pamoja na kujadili changamoto na namna bora ya kuwaandaa ili kufikia lengo , mashindano tunatarajia kuyafanya mwakani mwezi wa Ramadani

Mukhsin Mohamedi immamu wa Msikiti wa Forest Wilayani humo ,amesema kabla ya hatua yeyote kufanyika ,kwanza lazima waandaliwe wale wafundishaji wenyewe,watakaoandaa hayo mashindano

Yaani wale Walimu wausika wanaofundisha kwenye zile madrasa,watafutwe kwanza ,kwa sababu ile Quraan nimeisikiliza ilivyokuwa inasomwa na wale wasichana,ni Quraan iliyokwenda shule ,kwa hiyo tusipofanya maandalizi ya Walimu wenyewe itakuwa mtihani

Kwa hiyo tuwandale Walimu wenyewe watakao hifadhisha hiyo Quraan,baada ya kupata hao Walimu,tuakae sasa tuangalie ni jinsi gani ya kuwapata hao wanafunzi ambao watafundishwa hiyo Quraan

Lakini bila kufanya hivyo tutaandaa mashindano kweli mashindano kila kitu na gharama tutatumia kubwa ,lakini wale watoto watakachokisoma tofauti na tulichokusudia

Mwanamvua Kipingu,Katibu wa Jumuhiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA), Wilaya ya Siha,amesema baada ya kuhudhuria na kuona mashindano ya usomaji Quraan kimataifa ya Wanawake yaliyofanyika uwanja wa Benjamin Mkalipa Dar es salam

Amesema amejifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuona Quraan ikisomwa vizuri ,nakutamani kuona Wana Siha wanafanya mashindano kama hayo,kuanzia ngazi ya Wilaya,Mkoa, Taifa na Kimataifa.

Kwa hiyo sheikh wetu na Waumini waliokuwepo tujiandae ,tuanze kufanya mchakato tutafute Walimu bora tujifunze madrasa kusoma vizuri,ili tuweze kuingia kwenye mashindano makubwa,tumeona walifika uwanja wa mkapa kushuhudia mashindano walipata zawadi mbali mbali ikiwamo Pikipiki, Bajaji,simu na Gari.

Mashindano hayo kimataifa yalifanyika uwanja wa Mkalipa hivi karibuni na kuhudhuria na Nchi 11 Duniani ikiwamo Marekani na Urusi,ambapo mahindi wa kwanza alitoka Nchini Algeria

Mwisho