Site icon A24TV News

CCM Siha wajipanga kushinda uchaguzi wa Serikali za mitaa

Na Bahati Siha .
Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM), mkoani KilimanjaroMercy Mollel amewataka Wanachama wa chama hicho Wilayani mkoani hapa ,kujipanga vizuri ili kuweza kupata ushindi nguvu katika uchunguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika hivi karibuni na

Aidha amewataka Wanachama pamoja na Wananchi hao kujitokeza kujiandikisha katika Dafutari la kudumu la wapiga kura kuanzia September 25 hadi October 1 mwaka huu ,

Pia October 11 hadi October 10 mwaka huu kunazoezi lingine kujiandikisha kwenye Daftari la mkazi kwa siku 10 ambalo unajiandikisha kwenye kitongoji chako

Akizungumza na Wanachama pamoja na Viongozi wa chama hicho katika Kijijii cha Loigwa kata ya Donyomurwak,katika ziara yake ya siku tatu,amesema hawata shinda bila kufanya maandalizi ya kuwa na sifa

“Ni kweli bila kufanya maandalizi hatujapata ushindi,ushindi wetu lazima tujiandae vizuri Kwa kuwa na sifa “amesema Mollel.

Mollel amesema amekuja kwenye kata hiyo Kwa lengo la kukumbushana mambo muhimu yaliyopo mbele yetu katika kuelekea kufanya uchanguzi wa Serikali za mitaa

Amesema, mmoja ya jambo hilo ni kujiandikisha katika Daftari la wapiga kura,ili uwe na sifa ya kupiga kura na kuchagua kiongozi mzuri,kama nilivyosema litaanza September 25 hadi October 1 mwaka huu ,ina maana usipojiandikisha unakuwa hauna sifa ivyo kusababisha kukosa sifa ya kuchagua.

Nyote mnatambua kwamba Kila baada ya miaka mitano Kwa mujibu wa katibu ya Nchi yetu ni lazima tufanye uchunguzi uchaguzi huu ni muhimu sana kuliko chaguzi wa mwakani ,nisikilizeni vizuri , uchanguzi huu ni muhimu sana

Mollel Amefafanua kwa nini uchanguzi huu ni muhimu ,ni muhimu kwa sababu ndiyo utakao wapa taswira ya kuendea kwenye uchaguzi wanakwenda kufanya 2025,wa kupata Madiwani, Mbunge na Rais

Yaani huu uchanguzi wa Serikali za mitaa ndiyo msingi wa nyumba yetu , msingi ukijengwa vibaya nyumba hauwezi kusimamia,nasema uongo

“Nyumba hauwezi kusimamia ,yaani ili ni darasa,Sasa huu msingi wa Darasa hili kama haupo vizuri nyumba hii hauwezi kudumu kwa sababu nyumbani ni msingi”amesisitiza Mollel

Kwa upande wake katibu wa CCM , Wilayani humo Aly Kidunda,ametaka Wanachama Wilayani humo kuendelea kuwa na umoja na ushirikiano ndiyo msingi wa ushindi.

Pia akiwaonya wale ambao wanaanza kampeni kabla ya muda hajafika, kwamba hatua za kinidhamu zitachukuluwa dhidi yao

Mwisho