Site icon A24TV News

Fainali ya mashindano ya West Champion Ligi kuitimishwa September 15 mwaka huu

Na Bahati .Siha

Mashindano ya West Champion Ligi yanatarajiwa kufikia tamati September 15 mwaka huu katika uwanja wa kilima hewa Matadi Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro

Timu zitakazo cheza Fainali hiyo ni Timu ya Roseline kutoka West Kilimanjaro Wilayani humo na timu ya Kware fc kutoka Wilayani Hai mkoani hapa

Ambapo mgeni rasmi atakuwa Antony Mallya mdau mkubwa wa maendeleao Wilayani humo, mashindi wa tatu mechi yao itachezwa September 14 Mwaka huu, kati timu ya Nafco na Zinduka Fc kutoka Wilaya Siha.

 

Eli Pius mwanzilishi wa lig hiyo Akizungumza na waandishi wa habari,amewataka Wananchi Wilayani humo, kujitokeza kwa wingi kwenye faina hiyo kuja kuona burandani

Ambapo pia amesema siku hiyo ya Fainali mbali na burudani ya kabumbu ,kutakuwa na wasanii mbali mbali wakitoa burudani ,hakuna kiongilio,Wananchi wajitokeze Kwa wingi kuja kujionea wasisubiri kuja kihadhisiwa

Kwa upade wake Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro Hassani Karata,amesema michezo ni burudani,michezo ni ajira na michezo inasaidia kuimarisha Afya.

Awali Erick Joshua ,katibu wa bodi ya wadhamini West Champions Ligi amesema mashindano haya yalianza julay 28 mwaka huu na timu 16 zilishiriki mashindano hayo mbili kati ya hizo zilitoka wilaya ya Hai mkoani hapa

 

Mwisho