Site icon A24TV News

ISSA CHANDO JELA MAISHA KWA KUBAKA WA WATOTO WAWILI WADOGO .

Bahati Siha,

Mahakamani ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro September 12 mwaka huu,imemuhukumu kwenda jela Mkazi wa Majengo SanyaJuu Wilayani humo,Issa Chando( Meleki) (53),mkulima kutumikia kifungo cha Maisha kwa kosa la kubaka watoto wa miaka (6) wakazi wa Majengo

Mwendesha mashitaka wa Serikali Kurwa Mungo mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo Jasmine Abdul amesema tukio hilo lilitokea January mwaka huu kwa nyakati tofauti likifanyika nyumba kwa mshitakiwa

“Ni kweli alikuwa akiwaingiza kwa wakati mmoja kwenye nyumba yake nakuwafanyia ukatili huo uku alifahamu kufanya hivyo ni kosa”amesema Kurwa

Akielezea kwa undani kuhusu tukio hilo amesema siku moja wakati mzazi akimuogesha mtoto wake aligundua alikuwa akisikia maumivu sehemu za siri,ambapo mzazi huyo alihisi kwamba mtoto anauguwa ugonjwa wa U.T.I ambapo alichukuliwa jukumu la kwenda kununua dawa

Lakini kuna mtu alimwambia kwamba amuchunguze kwanza kabla ya kwenda kununua dawa ,kwani kunataarifa kuwa mtoto huyo amekuwa akiwafanyia ukatili mtoto na mtu mmoja ,ndipo walipochukua hatua ya kwenda kupima hospital na kugundua kuwa mtoto amekuwa akibakwa

Na walipomuhoji alimtaja mshitakiwa kuwa amekuwa akimchukua yeye na mwenzake na kuwaingiza nyumbani kwake na kuwabaka mara kwa mara na kuwapa zawadi na kuwatishia wasimueleze mtu

Kurwa amesema kitendo alichofanya ni kinyume na kifungu namba 130 (1)(2)(e)na 131(2)cha Sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 Kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022,

Ambapo kesi ya kwanza namba 1707/2024 ilikuwa na mashahidi 5 akiwamo Daktar na muhanga mwenyewe na kesi ya pili namba 1708/2024 ilikuwa na mashahidi 6 akiwamo mama mzazi pamoja na Mwenyekiti wa kitongoji

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo Hakimu ,alimtaka mshitakiwa kwamba analipi la kuimbia Mahakama ,ambapo aliomba Mahakama kumuonea huruma kwani ni visa vilivyotokana wazazi wa wahanga waliomba kupangisha katika nyumba yake na aliwanyima kwa sababu ni wavuta bangi ndiyo visa pia aliomba mahakamani kifungo cha nje

Hata hivyo Hakimu ilisema kutokana na kosa hilo kutokuwa na mbadala wa adhabu zaidi ya kifungo kutokana na umri wa wahanga kuwa miaka (6)

Na pia kukithiri kwa vitendo hivyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hivyo mahakama inakuhukumu kwenda jela kutumikia kifungo cha maisha jela

“Ni kweli vitendo vya ubakaji na ulawiti vinazidi kuongeza ndani ya Wilaya yetu na sehemu nyingine ili iwefundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo unakwenda kutumikia kifungo cha Maisha jela”amesema Jasmine.

 

Mwisho .

Mwisho