Site icon A24TV News

JESHI LA POLISI NCHINI LAMTAMBUA NA KUMPONGEZA ASKARI WP 6567 CPL SHEILA MENGO MWAKALEJA KWA UMAIRI WAKE

JESHI LA POLISI NCHINI LIMEMPONGEZA KWA NA KUTAMBUA KAZI YAKE NZURI YENYE UMAIRI MKUBWA BAADA YA KUSOGEZA BUS LILO PARK VIBAYA JIJINI ARUSHA .

AKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI DCP RAMADHANI NG’ ANZI AMESEMA KWAMBA Askari Polisi wa Kike aliendesha Basi WP Koplo Sheila nimempongeza kwa Niaba ya IGP kwa kuliletea sifa nzuri Jeshi la Polisi wakati akitekeleza majukumu yake ya Usalama Barabarani.

WAKATI HUO HUO AKIWA JIJINI ARUSHA KAMANDA NG’ ANZI AMEENDESHA OPERESHENI KABAMBE YA UKAGUZI WA MAGARI MABOVU . 

Arusha.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ramadhan Ng’anzi amefika Jijini Arusha na kufanya ukaguzi wa kushtukiza wa vyombo vya moto na kutoa onyo kwa baadhi ya madereva wanaotumia vilevi wakati wa kuendesha vyombo hivyo.

DCP Ng’anzi amebainisha hayo katika eneo la kisongo Jijini Arusha ambapo amesema kuwa katika kikao kilicho fanyika hivi karibu katika Shule ya Polisi Tanzania Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan alilitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha wanadhibiti ajali hapa Nchini zinazopoteza maisha ya watu wengi.

Aidha DCP Ng’anzi amesema kuwa operesheni hiyo ni endelevu na inafanyika nchi nzima huku akiwaomba abiria kutoshabikia mwendo na badala yake watoe taarifa kwa Jeshi hilo ili madereva wazembe wachukuliwe hatua za kisheria.

Mwisho .