Site icon A24TV News

JMAT YAPATA VIONGOZI WAPYA NI WAJUMBE WA KATA MBILI

Jumuhiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Wilayani ya Siha mkoani Kilimanjaro,wachagua wajumbe kata ya Ormelili na Songu

Jumuhiya ya maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro,imewatambulisha wajumbe wa kamati hiyo kwa Viongozi wa kata ya Ormelili na Songu Wilayani humo na kupewa majukumu.

wanayotakiwa kusimamia ikiwa ni pamoja kutunza amani na kuibua maovu kwenye jamii

viongozi wa kata hizo wakisema kwamba wajumbe hao wamekuja wakati muafaka na kwamba itasaidia kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya unyanyasaji kijinsia ikiwamo ubakaji na ulawiti na mimba kwa wanafunzi

Mbali na hilo pia itasaidia kuwadhibiti wauza madawa ya kulevya ikiwamo bangi na mirungi wanapofikishwa kwenye vyombo vya Sheria muda mchache wanaachiwa na kurudi mtaani kuendelea na biashara zao,sasa tunapoenda kwenye maridhiano lazima tuondoe kero hizo kwa wananchi

Wakizungumza mara baada ya utambulisho ya wajumbe hao kwenye kata ya Ormelili, wamesema kwa sasa wanafaraja kwa kuona Serikali imewaletea wajumbe hao na kwamba watawaunga mkono kufikia lengo la kutunza amani kwenye jamii.

“Ni kweli wajumbe wataongeza nguvu,hapa dhidi ya mapambano ya wahalifu wamechaguliwa wajumbe 13 Kwa kila kata ,watashirikiana na Polisi kata Mtendaji wa kata,Mwenyekiti wa vijiji na vitongoji pamoja na Diwani “Wamesema Viongozi hao

Polisi kata ya Ormelili Diomedes Mtayoba , Akizungumza mara baada ya kupata nafasi, amesema kata hiyo changamoto za uhalifu ambazo zipo kwa sasa kuna mimba kwa wanafunzi,kuozesha wanafunzi na kutelekeza familia,haya ndiyo matishio yaliyopo hapa,mengine ni utumiaji dawa za kulevye ikiwamo bangi na mirungi

Sasa tunapokwenda kwenye maridhiano lazima tuondoe kero ambazo zinawasumbua Wananchi,ukiangalia idadi ya uhalifu kama wizi umepungua Kwa kiasi flani raiti yake haipo juu sana kama matishio ya huu uhalifu nilio utaja

Kwa upende wao wajumbe wa kata ya Songu, Isaya Mkilindi amesema changamoto ya uhalifu katika eneo hilo ni ulevi wa kupingukia ,matumizi ya madawa ya kulevya ikiwamo bangi na mirung.

Ambapo wanadai anapokamatwa wuuzaji wa madawa hayo na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria muda mchache utawaona wamerudi mtaani na kuendelea na shughuli za uhuzaji wa madawa hayo

,Kitu ambacho kimekuwa kero kwa Viongozi na jamii ,kwani jitihada za kupambana dhidi ya uhalifu huo zinagonga mwamba ,hivyo kusababisha nguvu kazi ya Taifa kupungua na kurudisha juhudi za maendeleao nyuma ,kuja kwa Jumuhiya hii itasaidia kupunguza au kumaliza uhalifu

Awali Mwenyekiti wa Jumuhiya hiyo Gerald Mollel,amesema majukumu ya (JMAT)ni kutunza amani ,kuibua viashiria vya uvujifu wa amani , kushauri ,kuhakikisha kero zote zinafanyiwa kazi kwa mujibu wa Sheria,kupungua rushwa na mengine mengi

Leo tumewakabidhi wajumbe hao Kwa Uongozi wa kata akiwa Mtendaji,Polisi kata na Diwani wa eneo hilo,tunategemea ushirikiano ili kufikia malengo tuliokusudia ya amani Kwa Wananchi

Mwisho