Site icon A24TV News

Kata ya Livishi Wapewa angalizo Wasipojiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura

Na Bahati Siha .

Wananchi wa Kata ya Livishi Wilayani Siha
mkoani Kilimanjaro ,wametakiwa kujipanga vizuri ili kuweza kupata Viongozi wenye maono ya maendeleao katika uchunguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika November 27 mwaka huu

Haya yamejiri kwenye mkutano wa hadhara wa Kijiji cha Mowo njamu uliofanyika katika ofisi kijiji hicho na kuhudhuriwa na Viongozi mbalibali wa Serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleao ambapo ulijadili hangamoto na mafanikio ya eneo hilo.

Mtendaji wa kata hiyo, Elineema Mmari,Akizungumza katika mkutano huo amewataka Wananchi wa eneo hilo kuchagua viongozi watakao waletea maendeleao ya kukuza uchumi wa Taifa

Mmari amesema kabla ya kufika siku ya uchaguzi wa viongozi hao wa Serikali za mitaa November 27 mwaka,litatanguliwa na zoezi la kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura ambalo litaanza October 11 hadi 20 mwaka huu

“Ni kweli litaanza zoezi la kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura baada ya hapo litafuata zoezi la uchaguzi , tunatakiwa kuchagua viongozi wenye maono ya maendeleao,lakini uwezo kupata Viongozi hao kama haujajiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura tafsiri yake wewe hautaweza kupiga kura”amesema

Hivyo naomba Wananchi wa eneo hilo muda utakapofika wajiandikisha ukifika wafanye hivyo na ukifika muda kwenda kuchangia viongozi wajitokeze kwa wengi kutekeleza zoezi hilo umri kuanzia miaka 18 nakuendelea

Amefafanua kwa nini uchanguzi huu ni muhimu ,ni muhimu kwa sababu ndiyo utakao wapa taswira ya kuendea kwenye uchaguzi wanakwenda kufanya 2025,wa kupata Madiwani, Mbunge na Rais

Katika mkutano huo ,Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ambaye ni Afisa Tarafa Asteria Alfred ,amewataka Wananchi wa eneo hilo kuendelea na ushirikiano kuwana umoja na upendo kwani ndiyo msingi wa maendeleao.

Amesema hata kama mnachangamoto najua haziwezi kukosekana kwenye jamii ila jitahidini kuzitatua mwenyewe na msonge mbele kuleta maendeleao

Niwapongeze Diwani wa kata hii Lukus Nkini Serikali ya kijiji na Viongozi wote kw jitihada zao wanazozifanya kuleta maendeleao eneo hilo ikiwamo ujenzi wa zahanati nzuri na Miradi ya umwagiliaji

Tuendelee kuwatia moyo Viongozi wetu ,tusiwarudishe nyuma tunachokitaka sisi ni kwetu ni Maendeleao

Hata hivyo amewataka Viongozi wa Kijiji hicho kuitisha mkutano kwa wakati na kusoma mapato na matumizi na kuimiza Wananchi kupenda kuhudhuria mikutano inapoitishwa

Awali Wananchi wa Kijijii hicho wamemshukuru Rais Samia Suluhuu Hassani kwa kutumia fedha nyingine za Miradi ikiwamo za ujenga zahanati ambayo ipo mbio kukamilika itawasaidi kusogeza huduma karibu

Mmoja ya Wananchi hao ni Frida Mmari,ambeye amesema kukamilika Kwa zahanati hiyo,itasaidia kusogeza huduma karibu hasa kwa kina mama wanaojifungua,kwa hiyo niwapongenze Wananchi na wao kwa michango yao jitihada za ujenzi pamoja na Serikali

Mwisho