Site icon A24TV News

RAIS MWINYI: SMZ ITAENDELEZA JUHUDI ZA KUINUA VIPAJI KATIKA MICHEZO.

Na Mosses Mashala.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendeleza juhudi za kuimarisha Michezo kwa lengo la kuinua vipaji vya vijana.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 14 Sept 2024 katika Uwanja wa Gombani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kushuhudia Fainali ya Michuano ya Yamle Yamle kati ya timu ya Ponchinki City na Wete City.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amelitaka Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kuendelea kuimarisha Michuano hiyo ambayo sasa imekuwa na sura ya kitaifa na kuunga Mkono kila Mwaka.

Katika Mchezo huo wa Fainali timu ya Ponchink City imeibuka na ushindi wa Goli moja na kuwa mabingwa wapya wa Yamle Yamle.

Halikadhalika Dk.Mwinyi ameipongeza Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ kwa kuendelea kuwa Wadhamini Wakuu wa Michuano hiyo.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi alikabidhi zawadi mbalimbali kwa wachezaji waliofanya vizuri katika Michuano hiyo na kombe la Ubingwa kwa timu ya Pochinki City na Shillingi Millioni 20.

 

 

Mwisho .