Site icon A24TV News

WAKATAJI WA MITI HOVYO WAONYWA KUARIBU MAZINGIRA

Na bahati Hai.

wanaotoa vibali vya ukataji mit Wilayani i Hai waonywe kuchochea uharibifu wa mazingira
Jumuhiya ya watumia maji na uhifadhi wa mazingira mto Kware Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ,wamesikitishwa na utoaji wa vibali vya kukata miti bila kufuata utaratibu hivyo kuhujumu harakati za kutunza mazingira.

Hatua hiyo imekuja baada ya Jumuhiya hiyo kubaini miti kadhaa ikiwamo miruka na miringaringa imekatwa katika chanzo cha maji mto Kishenge kitongoji cha Maiputa Kata ya Masama Magharibi pembezoni wa Bondo la mama sawa,uku kibali kikionekana kutoka ofisi moja ya Serikali Wilayani humo.

 

Mwenyekiti wa Jumuhiya hiyo, Wilfred Masawe ,akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya kufika eneo la kingoji hicho cha Maiputa,ametaka watoa vibali hao kuzingatia utaratibu kabla ya kuvitoa vibali hivyo ili kutunza mazingira.

“Ni kweli tumekuta miti imekatwa lakini kibali wanacho na tulipokikagua tumekuta kimetoka ofisi za Serikali hii sio sawa wazingatie utaratibu wa kutoa vibali hivyo,

Masawe amesema wao wanajitahidi kusimamia vyanzo vya maji visiharibiwe kwa mujibu wa sheria lakini watu waliopewa dhima ya kutoa vibali wanatumia frusa hiyo kuharibu mazingira Kwa kutoa vibali hivyo,tunaomba Rais Samia Suluhuu Hassani kuangalia watu hao ili mazingira yabaki salama.

Amesema unakuta mtu amekata mti tena kwenye chanzo cha  maji na unapomuhoji ni kwanini unafanya hivyo,anakuambia ana kibali,na unapokiangalia kibali icho unaona kabisa kimetoka kwenye ofisi za Serikali, Sasa hii ni nini,inatukatisha tamaa

Kikubwa tunaomba wazingatia maadili ya kazi ili mazingira yabaki salama kwa kizazi cha sasa na kijacho,vinginevyo hii harakati za kupambana na uharibifu wa mazingira itakuwa kazi bure

Madina Mollel,amesema kazi ya usimamizi wa mazingira inachangamoto kubwa sana ,ikiwa ni pamoja na vitisho pindi wanapomkamata mtu ambaye ameharibu mazingira ,unapigiwa simu na kukupitisha kwamba achana na hilo jambo

Akitolea mfano siku moja walimkamata mtu katika chanzo hicho mto Kishenge,amekata miti aina ya mkufi,wakaambiwa kwamba mti ule ni ya Afisa mmoja wa Serikali,ambapo aliwapigia simu akiwatisha kuacha kufutilia jambo hilo,ili halipo sawa ,kazi hii ni ngumu.

Hi vyo tunaomba jamii iendelee kuunga mkono juhudi za Rais za Rais Samia Suluhuu Hassani mapambano dhidi ya utunzaji wa mazingira Kwa kizazi cha sasa na kijacho

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kitongoji hicho cha Maiputa Benson Ndos, amesema hilo jambo linaloendelea kutokea limempa mashaka ,kuona kinafanyika,wao kama viongozi wa Serikali ya Kijijii hatujashirikishwa ,nimesikia mashine zinanguruma zikikata miti

Mwisho.