Site icon A24TV News

waliorudi shule kutokana na changamoto Siha waishukuru Serikali

Na Bahati Siha .

Wanafunzi waliokatisha masomo kwa changamoto mbali mbali ikiwa pamoja na mimba za utoto ,Wamemshuru Rais Samia Suluhuu Hassani kwa kuwajali na sasa wanaendelea na masomo ili kufikia malengo waliyokusudia

Haya yamejiri wakati wa maazimisho ya Juma la elimu ya watu wazima yaliyofanyika kiwilaya shule ya msingi Sanya juu Wilayani humo na kuhudhuria na Viongozi mbalibali wa Serikali pamoja wadau wa elimu.

Wakizungumza mara baada ya kupata frusa,Wamesema nafasi waliyoipata wanamshukuru Mama Samia Suluhuu Hassani kwa kuona umuhimu wa wao kurudi shule na kuendelea na masomo

“Ni kweli tunamshukuru Mama Samia Suluhuu Hassani kwe nafasi aliyetupa ,maana hii nafasi ni ya bahati sana ,sisi kurudi kutimiza ndoto zetu kwa sababu zilishafifia kutokana na changamoto zilizotajwa”Wamesema.

 

Florens Lymo mmoja ya wanafunzi hao mkazi wa Kijijii cha Karansi Wilayani humo, amesema mwaka huu anafanya mtihani wa kidato cha Nne ,anasema baada ya kuruhusiwa kuendelea na masomo alianzia shule ya msingi Sanya kulikuwa na vyumba vya madrasa vilikuwa vimetengwa kwa ajili yao

Anasema alikuwa akitokea Kijijii hicho cha Karansi kufuata masomo kwa kutembea kwa miguu vipindi vinaanza saa tatu lakini yeye anafika shuleni saa saba kutokana na umbali

Florens amesema zilifanya juhudi za Serikali na kuhamia shule ya Sekondari Namwai na wenzake ,pale wanapata malazi ,chakula bure Walimu wanafundisha kwa moyo mkunjufu ,unaona ni jinsi gani mama anajitahidi kuona tunafaulu mambo ni mengi yanafanywe juu yetu ,kwenye Darasa lao wapo 27

Anasema changamoto nyingine wanasoma wakiwa Day wakipita barabarani wanapata maneno ya kejeli utasikia huyu bwana alishashindwa maisha ameamua kurudi shuleni na maneno mengi ya kejeli hatujakata tamaa

Katibu tawala wa Wilaya hiyo Jane Chalamila kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka,amewataka Wananchi wasiojua kusoma kujiandikisha kwenye vituo vya elimu ya watu wazima ili kuelimika na kupata frusa ya mipango iliyokuwepo kwa maendeleo yao na Taifa Kwa ujumla

Amesema tumeona katika Risala hali Halisi kunachangamoto nyingi ambazo zimekuwa zikijitokeza pamoja na programu hii kuwepo,licha Serikali kutaka Kila mtu kupata haki ya msingi ya kujua kusoma na kiandika

Tumeona kunaidadi ndogo sana ya wanafunzi wanajiunga katika hii mipango ukilinganisha na mahitaji.

Hivyo naomba nitumie jukwaa hili kuwaomba wadau wote wa elimu, Wazazi na walezi wajitahidi sana kuwahamasisha watoto ambao hawakuwza kufikia malengo yao kwa kukatisha masomo

Kwa wanafunzi walipata changamoto za kielimu, kutumia frusa hii zilizopo ili waweze kupata elimu kwa manufaa yao na vizazi vijavyo

Kwa sababu jambo alilofanya Rais Samia Suluhuu Hassani ni jambo nzuri sana ,zamani mtu akishakosa elimu mara ya kwanza alikuwa anajutia maishani mwake, lakini kwa sasa yake majuto hayapo tena

Hata hivyo wadau hao wa elimu wametoa angalizo kwa wanafunzi kuacha kuhadaika na vizawadi vidogo na kujikuta wanapata ujauzito wasubiri hadi waitimu masomo yao na mtu akiwanyanyasa watoe taarifa Kwa vyombo usika

Mwisho