Site icon A24TV News

WATUMISHI WA JIJI LA TANGA WAFURAIA KUKUTANA NA MKURUGENZI WAO KIKAO KAZI ,WAELEZEA CHANGAMOTO

Na Geofrey Stephen Tanga .

Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Mhandisi Juma Hamsini, akiwa na Menejimenti ya Halmashauri (CMT), leo Jumatano Septemba 18, 2024, amefanya kikao kazi na Watendaji wa Kata, Waganga Wafawidhi, Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu, chenye lengo la kufahamiana, kuweka mikakati ya pamoja, na kutatua changamoto za kiutendaji.


Katika kikao hicho, Mhandisi Hamsini amewataka viongozi hao kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati, na kwa kuzingatiwa kwa ubora, ili jamii inufaike na mipango ya Serikali ya kuwasogezea huduma kwa karibu.

Aidha amehimiza uwajibikaji kwa watumishi, na utoaji wa huduma iliyo bora kwa jamii.

Mwisho .