Na Bahati Siha .
Serikali Wilayani Siha imetakiwa kuweka muongozo mzuri wa bodaboda kufanya kazi ili kuweza kuwadhibiti na kupunguza matendo mbali mbali ikiwamo ya ajali za mara kwa mara barabara
Siha,
, Jamuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania(JMAT ),Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,imetoa rai kwa Serikali Wilayani humo kuwawekea utaratibu mzuri madereva badoboda ikiwa ni pamoja kuwa na katiba ili kupunguza uhalifu na ajali za mara kwa mara
Haya yamesemwa na makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Wilayani humo Idrisa Mndeme mara baada ya kutembelea vituo vya bodaboda ambapo alibaini baadhi ya vijiwe havina muongozo wowote unaowaongoza ambapo Kila mtu anajiamulia jambo lolote na kufanya
Akizungumza na waandishi wa habari Sanya Juu wilayani humo ,mara baada ya kutembea vijiwe vya bodaboda ameomba Serikali kuwawekea utaratibu wa kuwa na katiba itakayo kuwa muongozo wakati mwingine na kupunguza ajali za mara kwa mara ambazo zinasababusha vifo na majeruhi
“Ni kweli kuwa na katiba ni jambo jema ,kwani itawasaidiwa wao katika kutekeleza majukumu kwa kufuata utaratibu waliojiwekea ,kama mtu amefanya kosa katiba itawaongo na kama kuna mgeni amekuja kwenye kijiwe atapewa utaratibu “amesema Idrisa
Idrisa amesema amelazimika kutembelea vijiwe hivyo ili kufahamu vinaavyojiendesha kutokana na matukio ambayo yametokea hapa na pale ya watu kuumia na wengine wanajulikana ni bodaboda lakini kumbe sio,uhalifu, utumiaji dawa za kulevye ikiwamo bangi na mirungi na mambo mengine mengi
Amesema baadhi ya vijiwe hivyo vinafanya kazi kwa mazoea havina katibu kuwa havina muongozo wowote ,watu wanakuja wanapanda pikipiki na kupelekwa ,hivyo hata inapotokea tatizo sio rahisi kubaini kuwa limetokea kijiwe gani
Aidha amesema katika vijiwe alivyotembelea 10 vya kata ya Sanya juu ni pamoja na kijiwe cha kituo cha sheli ya kwa Mosha,kijiwe cha barabarani inayoelekea mahakama ya mwanzo SanyaJuu, Rex, Masaki na jiwe jeupe ,baadhi hivyo viwili vina katiba lakini haufutwi,hivyo ameomba Serikali isimamie zoezi ili wawezo kupata muongozo
Mwenyekiti wa bodaboda Wilayani humo Aron Japheth ,mesema changamoto ni nyingi kwa madeva hao wa bodaboda, ikiwamo kutokuwa na muongozo ,ulevi ,wezi na utumiaji dawa za kulevya na ,pamoja na mwendo kasi ambao mara nyingi unasababisha ajali
Amesema katika jitihada za kukemea mambo hayo lakini bila mafanikio, ,hivyo ameshukuru kwa (JMAT), kwa kuliona hilo na kutaka madereva kuwa na muongozo Kwa kushauri Serikali kusimamia zoezi hilo
Mwisho