Site icon A24TV News

JUMUHIYA YA WAZAZI SIHA YAPEWA KONGOLE KWA KUANZISHA LIGI MPIRA WA MIGUU

Na Bahati Siha .

Jumuhiya ya Wazazi CCM Wilayani Siha,wapewa Kongole Kwa kuanzisha Ligi ya mpira sambamba na kutangaza miradi iliyoletwa na Mama Samia Suluhuu Hassani.

Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Christopher Timbuka ameipongeza Jumuhiya ya Wazazi wa chama cha mapinduzi (CCM), Wilayani humo kwa kuona umuhimu wa kuenzi kazi zinazofanywa na Rais Samia Suluhuu Hassani kwa kuiitangaza kupitia michezo.

Haya yamesemwa wakati wa ufunguzi wa Ligi ya Samia Wazazi Siha Cup iliyofanyika katika uwanja wa CCM Sanya juu ambapo michezo mbali mbali ilizinduliwa ikiwa ni pamoja na mchezo wa mpira wa miguu na Drafti kwa Wanawake na Wanaume mgeni rasmi alikuwa Mkuu huyo wa Wilaya

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa michezo hiyo ,amewapa kongole Jumuhiya hiyo kwa kuandaa jambo hilo la kusifu na kuenzi kazi zilizofanywa Rais ndani ya wilaya hii

“Ni kweli nawapa kongole kwa kuliona hilo,kwa kusifu na kuenzi kazi zinazofanywa ndani ya Wilaya yetu na Rais Samia Suluhuu Hassani,kwa kupitia michezo kuzitangaza, ujenzi wa vituo vya Afya , Barabara,miradi ya maji”amesema Timbuka

Ni jambo zuri wamelifanya ndiyo maana mawasifu na waendelee na moyo huo wa kutangaza miradi iliyoletwa Wilayani humo kwa Wananchi

Lakini pia juhudi za michezo ,kutambua michezo ni Afya ,michezo inaleta Urafiki na Udungu, lakini pia inaimarisha Afya,najumbuka tulisisitizwa sana tufanye mazoezi ya mara kwa mara ili kujiepusha na magonjwa yasiyo ambukiza ,kwa hiyo michezo ni sehemu mojawapo ya tiba

Awali Mwenyekiti wa Jumuhiya hiyo Meijo Laizer,amesema lengo la michezo hiyo ni kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Samia Suluhuu Hassani kwa kazi nzuri ambazo anazozifanya.

 

Lakini kwa namna alivyohimiza maswala ya michezo na sisi kama Jumuhiya ya Wazazi tuka sema tumuunge mkono Rais wetu lakini kuhakikisha kwamba vijana wanapata frusa ya kuonyesha umahiri wao katika swala la michezo

Katibu wa Jumuhiya hiyo, Abdullah Chumu,amesema kupitia michezo hiyo,watahamasisha watu kujitokeza na kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi ili wawe na sifa ya kuchagua Viongozi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika November 27 mwaka huu

Ambapo amesema ili uwe na sifa ya kupiga kura na kuchagua Viongozi unaowataka wa kukuletea maendeleao lazima ujiandikishe kwenye Daftari la wakazi ambalo zoezi la kujiandikisha litaanza October 11 hadi 20 mwaka huu

Kwa hiyo kama vijana na wenzetu tunakutana kama sehemu ya kukumbushana kwamba kuna ratiba ya kujiandikisha , kuanzia miaka 18 na kuendelea

Mwisho