Site icon A24TV News

katibu wa Jumuhiya ya Wazazi (CCM), Wilayani Siha,awasihii vyama vya siasa kuweka mawakala katika uandikishaji wa Daftari la wakazi

Na Bahati Siha .

,Katibu wa Jumuhiya ya Wazazi wa chama cha mapinduzi (CCM), Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro Abdulla Chumu,amesisitiza vyama vya siasa Wilayani humo,kuweka mawakala kama utaratibu unavyotaka ili kuepuka malalamiko baadaye

Haya yamejiri katibu huyo alipotembelea vituo kadhaa katika zoezi la uandikishaji majina katika Daftari la wakazi kwa ajili ya uchanguzi wa Serikali za mitaa November 27 mwaka huu ambapo amekuta wakala wa CCM pekee kwenye vituo

Akizungumza mara baada ya kutembea katika kituo kujiandikisha Kijiji cha Sanya hoyee ,amawasii vyama hivyo kufahamu umuhimu wa kuweka mawakala katika vituo ili kuja kuwatambua wanajiandikisha.

“Kweli nimepangiwa maeneo ya kuzunguka kwa lengo kukagua maendeleao ya uandikishaji,lakini pia kukagua mawakala wetu wa CCM , mawakala wa vyema vingine sijawaona Sasa sijui hawajatamvua umuhimu wake”amesema Chumu

Chumu amesema,Vituo vya uandikishaji vipo 169 Wilayani humo na wameweka mawakala sehemu zote,mpaka sasa amesema amezunguka vituo 32 toka Asubuhi alivyopangiwa haijaona wakala wa chama chochote zaidi ya CCM

Sasa naomba niweke vizuri ,hawa mawakala kiutaratibu msimamizi wa uchanguzi aliwaandikia barua vyama vyote kuwasilisha mawakala wao katika zoezi la uandikishaji katika Daftari la wakazi

Amesema lengo la mawakala wanakaa pale kwa ajili ya kuwatambua wanakuja kujiandikisha katika kituo kile ni wakazi wa eneo lile ,

Ndiyo maana kama wakala hajajiririsha hana uhakika na mtu anaweza kumwambia Afisa msimamizi wa uandikishaji ebu huyu tufahamu ukazi wake akajulikana balozi wake ni wa eneo gani wajkijiridhisha ndiyo anaandikishwa hii ndiyo kazi ya mawaka.

“Ni kweli kazi ya mawakala ni kufahamu kwamba huyu ni mkazi eneo lake au sio mkazi wa eneo ,sasa vyama vingine hawajaweka ,hatutaki usumbufu baadaye Kwa wapiga kura kwamba huyu hatumufahamu wakati wa kuwatambua ni kupitia kwa mawakala wao”anesema Chumu

Baada ya zoezi hili kufikia mwisho, November 27,tunaenda kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa watu watajitokeza kupiga kura ,hatutarajii kusikia kwamba mtu huyo sio mkazi wa eneo ili ,kwani wao hawakuweka mawakala kuwatambua mapema amesisitiza Chumu

Hata hivyo msemaji wa chama kimoja cha siasa ambaye hakutaka majina yake yawekwe hadharani,amesema changamoto ni fedha kwenye vyama hivyo za kuweka mawakala sehemu zote na pia barua ya kuwaandaa mawakala ilichelewa kuwafikia wao

“Ni kweli changamoto ni hizo nilizozitaja,umuhimu wa mawakala tunafahamu hatuna jinsi fedha hakuna”amesema kiongozi huyo

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka,amewataka Wananchi kuendelea kujitokeza na kwenda kujiandikisha kwenye Daftari hilo ili kutimiza katibu na kuja kupata Viongozi wa zuri wa kuwaletea maendeleao

Mwisho