Site icon A24TV News

Madereva badoboda wavamia na kupasua kiyooo cha gari la Sheikh wa mkoa wa Kilimanjaro

Na BahatiHai,

Sheikh wa mkoani Kilimanjaro Shaabani Mlewa amelazimika kurudi nyumba Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro baada ya gari lake kupasuliwa kiyoo cha mbele na bodaboda eneo la Weruweru Wilayani Hai mkoani hapa

Mlewa alikuwa akielekea kwenye kilele cha maadhimisho ya fimbo nyeupe ambayo kitaifa inafanyika mkoani Kilimanjaro uwanja wa mashujaa, mgeni rasmi rasmi Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, amesema tukio hilo limetokea October 25 mwaka mchana eneo la Weruweru Wilayani Hai,akielekea katika maazimisho hayo ambapo alikutana na badoboda wengi wametanda barabarani na kurusha jiwe na kupasua kiyoo

“Ni kweli bodaboda wamerusha jiwe na kupasua kiyoo cha mbele, Hivyo kunilazimu kuahirisha safar ya kwenda kwenye maadhimisho hayo nakurejea nyumbani”amesema Mlewa

Mlewa amesema wakati wakielekea kwenye maadhimisho hayo mchana waliofika eneo la Weruweru Wilayani Hai,walikutana na msafara wa bodaboda wakielekea kuzika macheme lakini ghafla wakarusha jiwe Moja kwa moja likafika kwenye kiyoo cha mbele na kupasuka.

Sijaelewa lengo lao ,labda walikuwa wanashinikiza gari likae pembeni ili wao wapite sijui,lakini kushinikiza sio kwa mtindo huo

Amesema baada ya tukio hili Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amefika akiongozana na kamati ya usalama nakujionea hali halisi na ambapo alionyesha kukerwa na jambo hilo

Baadhi ya Wananchi wa Maeneo hayo akiwamo ,Julius Mrema wamelaani tukio hilo,wakisema bodaboda wanakwenda kuzika siku hizi wamekuwa kero barabarani

Wengi wao wamekuwa walevi,mwendo mkali ,ukikutana nao barabarani wanatanda barabara yote ,kwa kweli hawana ustaarabu Polisi wa barabarani wawachulie hatua ili iwe fundisho

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lazaro Twange, amesema anafutilia jambo ,na Shukuru kwa taarifa

Mwisho