Site icon A24TV News

NAIBU WAZIRI KIRUSWA AIPA KONGOLE BOT

Na Richard Mrusha Geita

NAIBU wa waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa ameipongeza Benki kuu ya Tanzania (BOT) Kwa kazi nzuri wanayofanya kwa kuendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wa madini na wadau mbalimbali kwenye sekta ya madini

Dkt Kiruswa ameyasema haya leo Oktoba 12, 2024 mara baada ya kutembelea kwenye banda la Benki kuu katika viwanja vya maonesho bombambili mkoani Geita.

kwa upande wake Sajent Rebecca Manase Afisa wa Jeshi la polisi kituo cha polis Geita akizungumzia huduma zinazotolewa na benki hiyo amesema amepata fursa ya kutembelea banda la Benki kuu ya Tanzania (BOT) kwenye maonyesho ya saba ya tekinolojia ya madini na ameweza kujifunza mambo mengi yenye faida na ya msingi.

Sajeti Rebecca amesema kuwa ametembelea kuona namna benki kuu wanavyofanya kazi lakini pia kujua juu ya matumizi ya noti na kuweza kuitambua noti ambayo haitumiki kiserikali.

“Nimeweza kufahamu zaidi juu ya matumizi ya noti na wananchi namna wanavyoweza kufaidika na benki kuu na kutambua noti ambayo haitumiki “amesema Sajeti Rebecca.

Ameongeza kuwa amepata elimu ya kutosha kutoka benki kuu hivyo amewaasa wananchi kutembelea banda hilo ili waweze kupata elimu.