Site icon A24TV News

TFS WADAU WA NYUKI TUMIENI VYEMA , MKUTANO MKUU WA DUNIA WA UFUGAJI NYUKI KUPATA MTANDAO WA UFUGAJI NYUKI WA KISASA

Na Geofrey Stephen  Arusha

KAMISHNA Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS),Profesa Dos Santos amewataka wadau wa ufugaji nyuki nchini kutumia fursa za mkutano wa Dunia wa Ufugaji wa Nyuki (Apimondia)unaotarajia kufanyika 2027 na kuvutia wawekezaji kwani ufugaji nyuki ni biashara ikiwemo ukuzaji wa utalii .

Profesa Dos Santos ameyasema hayo Jijini Arusha wakati wa mbio Nyuki marathoni zilizoshiirkisha wanariadha 500 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, Ulaya na Asia zenye urefu wa kilometa 10 na kilometa 21 zitakazofanyika kwenye Viwanja vya General Tyre Jijini Arusha.

Profesa Dos Santos akizungumza wakati wa               kukadithi misinga 20 ya nyuki kwa vijana wa                        wila ya arusha mjini 

Alisema utunzaji mzuri wamazingira utawezesha nyuki kuzaliana kwa wingu na kuwezesha uchumi kukua na kutoa rai kwa wananchi kufunga nyuki kwa kutumia mizinga ya nyuki kwani nyuki ni mtaji na mazingira lazima yalindwe.

Naye Rais wa Taasisi ya Nyuki Afrika,David Mukomana kutoka Zimbambwe, alisema mbio hizo zimefanyika Jijini Arusha kwalengo la kuweka sawa viungo vya mwili pamoja na kutangaza Mkutano wa Dunia wa Ufugaji Nyuki 2027(Apimondia )

Huku ,Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Woker Bees Africa, ( WBA) Restetuta Lopes Lazarus, alisema mbio hizo ni kuelezea umuhimu wa nyuki kwa maisha ya binadamu kutokana na umuhimu wake wanatupatia chakula ,asali ambayo ni tiba ya magonjwa mbalimbali ikiwemo kuboresha kumbukumbu na hiyo ni fursa kwa Wananchi kutunza na kuhifadhi mazingira .

Ambapo Meya wa Jiji la Arusha , Maximilian Iranghe alisisitiza kuwa mkoa wa Arusha unategemea kugawa mzinga ya nyuki milioni 2 leo katika mbio hizo za Nyuki marathoni mizinga ya nyuki zaidi ya 20 itagaiwa kwa makundi mbalimbali

“Tunataka Arusha iwe na nyuki wengi na Dunia kwa ujumla kutokana na utunzaji wa mazingira hivyo mkutano wa Epimondia 2027 utakuwa chachu katika kuleta maendeleo ”

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha Gerald Babu alisema mbio hizo ni chachu ya uhamasishaji wa ufugaji nyuki na kuongeza kuwa mbio hizo ni fursa kwa wafugaji nyuki na watanzania kulinda mazingira

Awali wanariadha 500 Kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, Ulaya na Asia walishiriki mbio za nyuki marathoni zenye urefu wa kilometa 10 na kilometa 21 zitakazofanyika Oktoba 26 kwenye Viwanja vya General Tyre Jijini Arusha.

Mbio hizo zililenga kuelezea umuhimu wa nyuki kwa maisha ya binadamu kutokana na umuhimu wake wanatupatia chakula ,asali ambayo ni tiba ya magonjwa mbalimbali ikiwemo kuboresha kumbukumbu na hiyo ni fursa kwa wananchi kutunza na kuhifadhi mazingira .

Washindi katika mbio hizo kilomita 21 k ni Nuru Benedicto akitumia muda wa saa 1:21:59 na wanaume mshindi alikuwa Mathayo Sombi akitumia muda wa 1:6:47 kutoka JKT
Mwisho