Na Bahati Hai .
Waumini wa Dini ya Kiislamu pamoja na Wananchi Wametakiwa kujitokeza kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi litaloanza October 11 hadi October 20 mwaka huu
Waumini wa Dini ya Kiislamu Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ,wametakiwa kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi ambalo ndiyo linawapa sifa ya kuchagua Viongozi wnaowataka wa kuleta maendeleao, katika uchunguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika November 27 mwaka huu.
Haya yamejiri kwenye Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhamedi (SAW), yaliyofanyika kiwilaya Msikiti wa Safii Bomang’ombe Wilayani humo,na kuhudhuria Waumini , Viongozi mbalibali wa Dini pamoja na Serikali
Muhamedi Msalu katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM), Wilayani humo,Akizungumza katika hadhara hiyo amewataka Waislmu na Wananchi kwa ujumla kujitokwze na kwenda kujiandikisha kwenye Daftari hilo la wakazi muda utakapo wadia
“Jambo kubwa ninaloweza kusema kwenye hadhara hii,ndugu zangu Waislmu, mwaka huu ni mwaka wa uchanguzi wa Serikali za mitaa,nitumie frusa hii kuwakumbusha vyote kuanzia October 11 hadi October 20 kutakuwa na uandikishaji wa Daftari la wakazi ambalo ndilo linakupa sifa wewe ya kuchagua.
Muhamed amesema kabla ya kufika siku ya uchaguzi wa viongozi hao wa Serikali za mitaa November 27 mwaka,litatanguliwa na zoezi la kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura ambalo litaanza October 11 hadi 20 mwaka huu
“Ni kweli litaanza zoezi la kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura baada ya hapo litafuata zoezi la uchaguzi , tunatakiwa kuchagua viongozi wenye maono ya maendeleao,lakini uwezo kupata Viongozi hao kama haujajiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura tafsiri yake wewe hautaweza kupiga kura”amesema Muhamed
Hivyo kuomba muda utakapo wadia Waislmu na Wananchi kwa ujumla kujitokeza Kwa lengo la kutimiza wajibu wa kikatiba
Sheikh wa mkoani Kilimanjaro Shabani Mlewa naye amesisitiza jambo hilo, amewaomba Waislmu na Wananchi muda utakapofika wajiandikisha ukifika wafanye hivyo na ukifika muda kwenda kuchangia viongozi wajitokeze kwa wengi kutekeleza zoezi hilo umri kuanzia miaka 18 nakuendelea
Nakuomba watu wenye sifa za kugombea wasisite kujitokeza muda utakapo wadia,nafasi za Mwenyekiti wa mtaa , Kijiji, kitongoji na wajumbe wa Serikali
Amefafanua kwa nini uchanguzi huu ni muhimu ,ni muhimu kwa sababu ndiyo utakao wapa taswira ya kuendea kwenye uchaguzi wanakwenda kufanya 2025,wa kupata Madiwani, Mbunge na Rais.
Kwa upande wake Fuya Kimbita ambaye alishakuwa Mbunge wa Jimbo la Hai,2005 hadi 2010 na pia kuwa mjumbe wa halmshauri kuu ya CCM Taifa (MNEC),ambeye alialikwa kwenye hadhara hiyo,amegusia mambo machache ikiwa ni pamoja na upendo
Akizungumza kwenye Maulidi hayo mara baada ya kupata frusa hiyo,ameomba upendo kudumishwa , upendo ukidumishwa haya mengine yatafuata, maendeleao yatakuja amani itakuwepo,kwanza upendo, kwa hiyo kikubwa nasisitiza upendo
Mwisho