Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdala Ulega amezitaka taasisi za Utafiti wa Uvuvi Tanzania kushirikiana kikamilifu na taasisi za kiserikali kuangalia uwezekano wa kupandikiza samaki katika bwawa la Mwalimu Julius Nyerere ili kukuza ustawi wa uvuvi nchini.
Ulega maeeleza kuwa kufuatia taifiti zilizo fanywa zinaonyesha uwezekano wa kuweka samaki katika Bwawa la Mwalimu Nyerere ni mkubwa na kwa kufanya hivyo kutachochea shuguli za kiuchumi kwa watanzania wa ukanda huo.
Waziri Ulega alitoa maelekezo hayo wakati akifungua Kongamano la Tatu la Kisayansi la Utafiti wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji katika Kukuza Uchumi wa Buluu Endelevu(3rdFAR4VIBE) linalofanyika Jijini Arusha kuanzia Oktoba 29 hadi 31, 2024. Mkutano uliyo shirikisha watafiti na wadau mbalimbali wa sekta ya uvuvi kutoka nchini 15 duniani.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Abdallah Ulega amesema pamoja na mafanikio yaliyoanza kuonekana kwenye ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba kwenye maziwa, ni muhimu sasa Watafiti wa masuala ya uvuvi kuanza kufanya utafti utakaosaidia kuweka mkakati na mpango wa matumizi bora ya maziwa hayo ili kuepusha malalamiko ya muingiliano baina ya wafugaji wa samaki na watumiaji wengine.
Amesema tafiti zinasaidia kuoata idadi kamili ya samaki pamoja na kujua mazingira ya samaki na amezielekeza taasisi za ZAFIRI na TAFIRI kufanya utafiti katika maeneo ya Ziwa Nyasa na Ziwa Tanganyika ili kujua idadi ya samaki iliyopo katika maziwa hayo ili kuwa na idadi sahihi ya kitafiti.
“Tunapo fanya tafiti tunategemea kuwa na majibu sahihi ya kile tunacho kifanya, Utafiti zaidi ufanyike katika kuangalia uwezekano wa kupandikiza samaki katika bwawa la Mwalimu Julius Nyerere ingawa hatua za mwanzoni zinaonyesha msisitizo mkubwa na kuwezekana”. Amesema Ulega.
“Wana sayansi wana kazi kubwa ya kufanya na kujua namna bora kupatikana kwa chakula cha samaki sambamba na upatikanaji wa vifaranga bora vya samaki ili kuleta matokeo mazuri kwa ustawi wa taifa letu. Ameongeza Ulega.
Naye Dkt. Edwin Mhede Naibu katibu Mkuu anayesimamia Uvuvi ndani ya Wizara ya Mifugo na uvuvi amesema kuwa, Kupitia taasisi ya utafiti kwa kushirikiana na vyuo vikuu pamoja na watafiti kutoka nchi 15 duniani kwa lengo la kufanya maboresho kwenye sekta ya uvuvi na kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi.
“Leo tunapokea tafiti mpya kutoka TAFIRI kuona ni wapi kwenye sera zetu tukaangazie namna ya kuboresha ili matokeo hayo yaende kugusa watu katika sekta ya uvuvi takribani milioni sita “.Amesema Mhende.
Mkurugenzi mkuu waTaasisi ya utafiti wa samaki TAFIRI. Ismail Kimerei,amesema kuwa Mkutano huo watatu wa Sayansi na Uvuvi wa Uchumi wa bluu endelevu.
Amesema watawasilisha matokeo ya utafiti katika maeneo Tisa ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi ,Teknolojia ya Ufugaji wa viumbe maji ,Usimamizi wa rasilimali katika bahari
Amesema katika kipindi cha miaka miwili wamefanya tathimini ya mtawanyiko wa Samaki katika bahari maziwa na mito.
Amesema Serikali imeweka mpango mkakati wa kuondoa 60% ya upitevu wa Samaki ifikapo mwaka2030.
Amesema uukosefu wa takwimu sahihi ni tatizo linalozitesa nchi nyingi duniani hivyo wanatengeneza mfumo ambapo Wananchi wenyewe kwenye mialo wanatoa taarifa za Samaki kwa kupiga picha.
Ameongeza kuwa teknolojia inawezesha kutambua maeneo yenye Samaki.na hivyo kumwezesha mvuvi kuvuka eneo lenye Samaki wengi.