Site icon A24TV News

WIZARA YA MADINI, FARU GRAPHITE WAJADILI CHANGAMOTO ZA MAENDELEO YA MRADI

Dodoma, Mtumba.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Oktoba 07, 2024 aliongoza kikao kati ya Wizara na Kampuni ya Faru Graphite Corporation kilicholenga kujadili maendeleo ya Mradi wa uchimbaji Madini ya Kinywe wa Faru Graphite unaotekelezwa katika eneo la Mahenge, Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma, Mbibo aliihakikishia kampuni hiyo kushughulikia changamoto inazokabiliana ikiwemo kifungu 56 na 10 cha Sheria ya Kodi ya Mapato, Sheria ya Madini na sheria zingine ili kuuwezesha mradi huo kutekelezwa kwa wakati.

Faru Graphite Corporation ni kampuni ya ubia kati yake na Serikali ya Tanzania ambapo Serikali ina umiliki wa hisa zisizofifishwa za asilimia 16 na kampuni ya Black Rock Limited yenye hisa asilimia 84

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Faru Graphite Corporation Bw. John de Vries na Mkurugenzi wa Black Rock Mining masula ya fedha Bw. Paul Sims alieleza kwamba kampuni hiyo imeweza kushughulia masuala kadhaa ikiwemo changamoto ya umeme na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi na uendeshaji wa mradi ili kuhakikisha unatekelezwa kwa wakati.

Pia, de Vries alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara ya Madini kwa ushirikiano inaoutoa katika kutatua changamoto zinazoikabili, na kuongeza kwamba, Wizara iendelee na ushirkiano

Mwisho .