Site icon A24TV News

ACT,Wazalendo wajinadi kupata ushindi uchanguzi wa Serikali za mitaa siha

Na Bahati Siha .

Siha,Chama cha ACT Wazalendo Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro kimetakiwa kuhakikisha kinaongeza idadi ya Wanachama kwa kusajili Wanachama wapya kwenye mfumo unaoitwa Act kiganjani ili kuweza kushinda katika uchunguzi wa Serikali za mitaa November 27 mwaka huu na uchunguzi Mkuu mwakani

Haya yamesemwa na Rachel Kimambo katibu uchumi Taifa wa chama hicho ,katika kikao kazi kilichofanyika Sanya juu Wilayani humo,na kukutana na Wanachama pamoja na wagombea watakaoshiriki uchunguzi wa Serikali za mitaa

Akizungumza na Viongozi wa chama hicho ngazi ya Wilaya pamoja na wagombea na Wanachama mara baada ya kupata frusa ya kunzungumza, amesema bila kuwa na Wanachama itatuwia vigumu kupata ushindi kwenye uchanguzi

“Naomba jambo moja kama sio mawili,jambo la kwanza ni muhimu sana kuhakikisha kwamba kila siku kutokae sasa tunaingiza ,tunaingiza watu wengine au kushawishi kuingia kwenye chama chetu “amesema Rachel

Rachel amesema wanaitaji kuwa na Wanachama wengi sana ili kufikia malengo tuliyokusudia ,hatuwezi kwenda kushinda uchunguzi ikiwa tukiwa kundi ndogo

ReKwa hiyo niwaombe sana ,sisi sasa hivi tuna mfumo unaoitwa Act kiganjani, hauwezi kudanganya kila mtu anayesajiliwa tunaweza kumuona makao makuu

Natamani kuona idadi ya Wanachama katika Jimbo hili la Siha inakuwa kubwa ,Kwa sababu kila jimbo lina idadi ya wapiga kura angalau ukifanikiwa kuwa na asilimia 10 ya hao watu tunaweza kuhakikisha tutafanya vizuri

Kwa hiyo mimi naomba sana kama nilivyoahidi tujitahidi kadri ya uwezo wengu kuhakikisha tunashirikiana na nyinyi kupata ushindi kuanzia ngazi za Serikali za mitaa hadi uchunguzi Mkuu mwakani

Kwa upande wake mjumbe wa halmshauri kuu ya Taifa Act kanda ya kasikazini Mdimu Ally ,amesema chama hicho kimekuja na sera mbadala,ni chama ambacho kinakuja na majawabu katika maeneo ambayo yamekosa ufafanuzi ni chama cha kimkakati.

Awali katibu wa chama hicho ngazi ya Wilaya Giliad Mmar,amesema wamejipanga kushinda uchanguzi huu wa Serikali za mitaa katika maeneo waliosimamisha wagombea kutokana na Sera watakazo zinadi kwa Wananchi

Tumejipange na mikakati ya kuhakikisha kupata ushindi ,lazima tuwe na mkakati ya kupata ushindi katika uchunguzi wa Serikali za mitaa November 27 mwaka huu , kwa kuzimulika changamoto za Wananchi zinazowakabili.

Mwisho