Site icon A24TV News

jeshi la Polisi Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, linamshikilia baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita kwa kosa kuchoma nyumba

Na Bahati Siha,

Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Christopher Timbuka, amesema wanafunzi kadhaa wa kidato cha sita shule ya Sekondari Sanya Day,wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa kuleta vurugu shuleni hapo ikiwa ni pamoja na kutaka kuchoma nyumba ya mwalimu

Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu,amesema tukio hilo limetokea November 17 ,2024,nakuwataka wanafunzi kuzingatia yaliyowaleta shuleni

“Ni kweli tukio limetokea la wanafunzi kutaka kuchoma nyumba ya mwalimu jambo ambalo ni la kuuzunisha na sasa wapo chini ya vyombo vya Sheria”amesema Timbuka

Timbuka anasema ,kuna wanafunzi alikutwa na simu siku hiyo hapo shuleni na walinzi walimuona na kumshitakia kwa mwalimu ,kitendo hicho hakikuwafuhisha wanafunzi

Baada ya kuona wameshitakiwa kwa mwalimu,wakaanza kuwarushia mawe Walinzi jambo ambalo lilizusha mtafaruki ,chanzo ndiyo hicho

Amesema baadaye usiku walikusanyika na kutaka kuchoma nyumba ya mwalimu, bahati nzuri nyumba iliungua kidogo Mlangoni,moto haukueneo maeneo mengine

Watu waliousika na wote wanajulikana na waliotenda ,waliousika ,kwa hiyo utaratibu wa kisheria unaendelea kuchukuliwa

Kikubwa nachotaka kuwaambia ni kwamba watambue nini kilichowaleta shuleni

Ili utambue kilichokuleta shuleni ,ni vema kutokujiusisha na mambo mengi,kutokwenda tofauti na Sheria na kanuni zinazoongoza shuleni

Sababu kama simu zinakatazwa,mtu anatakiwa kuzingatia,kama unatumia kipindi cha likizo tumia mpaka utakapo choka

Unapokuwa shuleni napenda watu wazingatie kanuni na Sheria zinazoongoza shule,watambue kilicho waleta shuleni

Wazazi wanapoteza gharama , Serikali inapoteza gharama wao wapate elimu, sasa wasipotumiza hiyo watakuwa hawajajitendea haki wao wenyewe au Wazazi wao na Taifa Kwa ujumla

Diwani wa kata ya Nasai,Haphurehi Kifum ,amesikitishwa na jambo hilo,na kuwaomba wanafunzi kuzingatia yale yaliyowafanya wao kuwa hapo katika eneo hilo

Wafuate maadili ya shule kwamba haruusiwe kuwa na simu shuleni hapo kwa mujibu wa Sheria

Wasubiri wakihitimu masomo yao wakirudi uraiani watazikuta nyingi,wakumbuke wanatoka sehemu mbali mbali ,mtu umefika kidato cha sita unafanya vitu kama hivyo haipendezi

Mwisho