Site icon A24TV News

KWA KURA ZA KISHINDO KIKUBWA UVCCM KIBOSHO MAGHARIBI YAMPATA MWENYEKITI WA VIJANA.

Na Mwandishi wa A24tv Kibosho

Uvccm imefanya uchaguzi wake wa kumchagua Mwenyekiti wa Vijana wa kata hiyo iliyoko wilayani Moshi ambapo wajumbe walimchagua Comrade Bosco Makoi kuongoza baraza hilo la Vijana kata

awali nafasi hiyo ilikuwa wazi baada mwenyekiti aliyekuwepo kujiuzulu.

Uchaguzi huo umesimamiwa na mkurugenzi wake ambaye ni katibu kata Ndugu.Mark Shio akishirikiana Mwenyekiti wa chama wa kata hiyo Cloude Olomi

Makoi amewashukuru wajumbe wote kwa kumchagua huku akia hidi kushirikiana na viongozi wenzake, kuunganisha Vijana pamoja na kuzisaka fursa mbalimbali kwa maslahi mapana ya Vijana wa Kibosho Magharibi bila kubagua itikadi ya vyama.