Site icon A24TV News

Naibu waziri wa Afya Godwin Mollel ,ameomba Wananchi katika uchunguzi wa Serikali za mitaa kuchagua Viongozi wa CCM ili asiaibike mbele ya Rais

Siha,

Zikiwa zimesalia siku mbili kwa kufanyika uchanguzi wa Serikali za mitaa November 27,2024,Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, Ally Kidunda ,ameomba Wananchi kuchagua Viongozi wa vijiji wanatokana na CCM

Hayo yamejiri kwenye kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Kijijii cha Merali kata ya Sanya juu Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro , ambapo walikusanyika wananchi kutoka sehemu mbali mbali ya Kijiji hicho kuja kusikiliza sera.

Akizungumza mara baada ya kupata frusa ya kuwanadi wagombea hao wakiwamo wa vitogoji ,amewataka Wananchi kuchagua Viongozi wanaotokana na CCM kwani wanamaona ya maendeleao na sio vingine

“Ni kweli msituchanganyie vitu vingine,Rais Samia Suluhuu Hassani tunaye
Mbunge, Godwin Mollel tunaye na Diwani Juma Jani tunaye,wote wanatokana ni wa CCM,Sasa tunatafuta Wenyekiti wa vijiji, vitogoji pamoja na wajumbe wa vijiji “amesema Kidunda.

Kidunda amesema lazima tuende sawa ,ili tochi iweze kuwaka lazima iwe na betr tatu,lakini ukichanganya na gunzi ukaliweka katikati tochi haiwezi kuwaka

Hivyo kwenye uchanguzi msituchanganyie na magunzi wote wenyeviti watoke CCM,litakuwa ni jambo jema sana,nawaomba sana Wananchi mfanye hivyo,siku ya jumatano kushokutwa tena ni siku ya mapumziko

Diwani wa kata hiyo Juma Jani, akizungumza kwenye kampeni hiyo, amesema Serikali itaweka lami Barabara
ya SanyaJuu kuelekea Merali hadi kwa alxzanda ,barabara hiyo imekuwa ikifanyiwa matengenezo mara kwa mara,lakini Serikali imeona bora kuweka lami

Amesema Mungu akipenda barabara ya kuanzia kituo cha mabasi ,inaelekea majengo nyati inaungana na barabara inayoelekea Makiwaru hadi kia inayojengwa na Tan road inawekwa lani,kwa hiyo taarifa ndiyo hiyo ,tuchagua wenyeviti kutoka chama tawala ,Mnashuhudia mafanikio tuliyoyapata katika kipindi cha miaka mitano, kama vile ujenzi wa barabara na masuala ya elimu..

Kwa upande wake Naibu waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo Godwin Mollel,amewaomba Wananchi kujitokeza na kuunga mkono wenyeviti wa vijiji na vitogoji pamoja na wajumbe kuwachagua kutoka CCM,ili asije kuaimbika mbele ya Rais Samia Suluhuu Hassani.

“Wangapi wanataka Mimi niaibike, naombeni mkawape hawa wenyeviti Uongozi ili Mimi nisiaibike “amesema Mollel

Amesema Serikali imetuma fedha nyingi za maendeleao katika Jimbo hilo,zikiwamo za , Barabara,vituo vya Afya,shule mbali mbali ikiwamo za ufundi,kwa kweli Wananchi endeleeni kuunga mkono juhudi za Serikali ili kuendelea kunufaika na miradi mbali mbali

 

mwisho