Site icon A24TV News

Siha yafanya vizuri yashika nafasi ya kwanza mkoani Kilimanjaro katika mbio za Mwenge

Siha,

Baraza la madiwani Halmshauri ya Siha mkoani Kilimanjaro limeomba mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijiji (RUWASA )Wilayani humo,wanapotekeleza miradi ya maji wahakikishe miundombinu ya mabomba inaingia kina kirefu ili miundombinu hiyo isiweze kuharibiwa wakati mitambo ya inayotengeneza barabara I siweza kufikia na kuharibi Maeneo hayo

Haya yamejiri kwenye Baraza la kawaida la madiwani wa halmshauri hiyo lilifanyika katika ukumbi wa halmshauri hiyo na kuhudhuria na Wadau mbalibali wa maendeleao wakiwamo Viongozi wa Dini.

Katika taarifa yake aliyoitoa katika Baraza hilo November 22 mwaka huu,Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Dancani Urasa,ametaka RUWASA kuzingatia utaratibu huo ili kuepuka gharama zisizo za lazima ya kununua mabomba mengine baada ya hayo kuharibiwa

RUWASA watusaidie kwenye swala wanapotekeleza miradi yao ,miradi ambayo imepita kwenye eneo la barabara ,kitu cha kwanza ni kuweka alama , kuonyesha pale kuna Bomba limepitisha maji

Lakini pia wanapoweka hiyo miundombinu wahakikishe kwamba miundombinu inaingia kina cha chini ambacho akati barabara inatengenezwa ile mitambo inayotengeneza barabara haiwezi kufikia na kuharibu hayo maeneo

Nimekuwa nikipata malalamiko kutoka kwa Wananchi wakidai kwamba miundombinu ya maji imekuwa ikiharibiwa kwa mabomba kukatwa wakati barabara za vijiji zinapochimbwa kwa ajili ya matengenezwa na hivyo kusababisha kukosa maji na kuingia hasara ya kununua mabomba mengine

Hivyo nawaomba RUWASA wanapotekeleza majukumu yao wajitahidi wazingatie utaratibu huo ,ili kuepuka gharama zisizo za lazima.

Pia katika taarifa yake amesisitiza swala la utunzaji wa Barabara ,tuendelee kuwatambia Wananchi wetu wasipitishe mifugo Barabarani , Diwani wa kata ya Gararagua asaidie Barabara ya iliyojengwa kwa kiwango cha lami na Tan road kutoka Kwa Dc,kuelekea Karansi,nivizuri wakatafuta njia nyingine ya kupitisha mifugo yao kwani Barabara hiyo itaharibika

Aidha amewataka Wananchi kutunza vyakula kutokana na hali ya hewa ilivyo sio nzuri ,na kusisitiza Wananchi kupanda mzao yanayostahimili ukame ikiwamo mihago mazao ya muda mchache kama maharage

Sambamba na hilo ameomba wataalumu kuendelea kusimamia miradi ya maendeleao,tumepata fedha nyingi sana ,tunao Mradi wa kituo cha Afya lawate pamoja na shule amani inayojengea Indumet, tuendelee kusimamia miradi vizuri

Lakini pia naipongeza ofisi ya Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri ,Ofisi ya mkuu wa Wilaya,watumishi pamoja na Wanasiha,kwa jinsi ambavyo mapokezi ya Mwenge wa uhuru mwaka huu, Wilaya ya Siha imekuwa ya kwanza kimkoa imefanya vizuri kati ya wilaya sita,tunatamani mwakani tuwe wa kwanza Kitaifa,tufanye vizuri zaidi

Kwe upande wake Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Haji Mnasi , amesisitiza kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa November 27 mwaka huu,watu kujitokeza kwa wingi,kuchagua Viongozi wanaowapenda

“Ni kweli zimebaki siku chache chondochondo Viongozi madiwani tuwahimizi Wananchi wetu kujitokeza kwa wingi wiki ijayo ni siku ya mapumziko ili kupiga kura “amesema Mnasi

Mwisho