Na Bahati Siha
,Zikiwa zimesalia siku 16 kabla ya uchanguzi wa Serikali za mitaa November 27 mwaka huu, Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,wameombwa kuweka kando shughuli zao siku hiyo ili kujitokeza na kuchagua Viongozi wazuri
Haya yamesemwa na Diwani wa kata ya Sanya juu Wilayani humo Juma Jani, kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo hilo Godwin Mollel kama mgeni rasmi,wakati wa maonyesho ya usomaji Quraan pamoja na masomo mengine wanafunzi wa Madrasa SanyaJuu Wilayani humo.
Akizungumza na Viongozi mbalibali wa Serikali na Dini pamoja na wazazi na walezi wa wanafunzi hao mara baada ya kupata frusa, ameomba siku hiyo watu kuweka kando shughuli zao na baada ya kupiga kura waendelee na shughuli zao kuwaingizia kipato
Jani amesema Uchanguzi wa Serikali za mitaa unepangwa kufanyika November 27 mwaka huu,ambapo Rais Samia Suluhuu Hassani ametangaza siku hiyo ni ya mapumziko ili Wananchi wajitokeze kupiga kura na kuchagua Viongozi hao
“Ni kweli siku hiyo Rais Samia Suluhuu Hassani,amesema ni siku ya mapumziko ,na sisi katika shughuli zetu tumuunge mkono baada ya kupiga kura tunaweza kuendelea na mambo yetu”amesema Jani
Sasa shime Wanaume shime, wanawake ,November 27 mwaka huu tunaenda kuchagua Viongozi,usingoje kuja kulalamika ,kuna watu wakati wa uchanguzi wanajifanya wanashughuli nyingi sana ,wanamambo mengi sana na kushindwa kushiriki uchanguzi
Lakini anapopata jambo anakimbilia kwa kiongozi ambaye yeye hakumchagua,ikatokea bahati mbaya jambo lake likakutana na magumu ,hapo Sasa anaanza kulalamika,katoka wapi huyu ni wanani ,majitu yaliyochaguliwa hapana nenda kuchagua kiongozi muwanibikaji ,amesisitiza jani
Kwa hiyo niwaombe ndugu zangu November 27 nendeni mkachague Viongozi watakao waletea maendeleao,wa Kijijii, kitongoji na watumbe wahalmashauri ya Kijijii
Baada ya hapo tuembe uzima Mwenyezi Mungu akipenda akitupa uhai tuende tena Tukapate Rais,Wabunge na Madiwani mwakani.
Mbali na hilo amesema kwamba Risala iliyosomwa ya mgeni rasmi anaipeleka kwa muusika ili iweze kufanyiwa kazi,
Sheikh wa Wilaya hiyo AbubakaHashimu,ametaka kusomwa elimu zote ,elimu ya mazingira na elimu ya Dini ,ambapo amewapongeza waandaaji wa maonyesho hayo pamoja na mwalimi wa Madrasa hiyo kwa kuona umuhimu wa kuwapa wanafunzi elimu ya Dini
Amesema elimu ya Dini ni muhimu sana inasaidia kuwalea na kuwafundisha wanafunzi tunu ya misingi ya maishani ya Imani, maadili na utu dhidi ya mmonyoko wa kiutu na kimaadili unaoendelea kuikumba jamii ili ibaki salama
Abubakar amesema elimu ndiyo inakupa mwangaza wa kuonyesha njia sawa na kuonyesha njia mbaya,Kwa hiyo wiazazi na walezi ili kupata wetu wema katika Nchi hii wakataa rushwa ni lazima wapete elimu ya Dini ili iwe muongozo kwao.
Mwisho