Na Bahati Siha .
Siha,Wanafunzi wa shule ya Msingi lemosho kata ya Indumet Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko ikiwamo kipindu pindu kutoka na kukosa maji safi na salama shuleni hapo
Maji hayo yalikatwa na Bodi ya maji Magadini Makiwaru Kwa madai ya kudai bili ya maji zaidi ya sh,1milioni ,uku wadao wa elimu wakiomba Serikali kuchimba visima kwa kila shule kuepuka kadhia hiyo
Wakizungumza na waandishi wa habari Kwa nyakati tofauti,Wamesema wanafunzi hao wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko ikiwamo ugonjwa wa kipindu pindu nakuomba Wadau wa elimu kuingilia kati swala hilo
“Ni kweli wapo hatarini kupata magonjwa hayo ikiwamo kipindindu pindu na UTI,kutoka na vyoo wanavyotumia vya kisasa kuitaji maji mengi ili kuwa na usafi ndiyo hayo yamekatwa”Wamesema
Erinest Shirima mmoja ya wanafunzi wanasoma shule hiyo, amesema maji yamekatwa shuleni hapo toka June mwaka huu,Sasa ya kudaiwa bili ya maji,hivyo kusababisha wanafunzi kutesema kwa kukosa maji
Amesema busara ingetumika ili maji yaendelee kuwapo kuliko kukata,kwani madhara yake ni makubwa kwa watoto kupata magonjwa ikimo kipindindu na UTI,na kuongeza gharama za kwenda hospital kupata matibabu
Anna Judika mkazi wa Matadi amesema shule hiyo yenye wanafunzi 1300 ,wanafunzi wanakunywa maji ya mfereji baada ya maji ya bomba safi na salama kukatwa katika shule hiyo,hivyo kuomba wazazi kuangalia jambo hilo ili kunusuru na magonjwa mbali mbali yanayotokana na ukosefu wa maji safi na salama
Hata hivyo mwalimi Mkuu wa shule hiyo Raymond Lengereri ,alipoulizwa kuhusu kukatwa kwa maji shuleni hapo,alikanusha na kudai kwamba maji yapo na hayajakatwa
Diwani wa kata hiyo Vicent Kileo, akizungumza kuhusu jambo hilo,amesema kweli bili ya maji ipo na inadaiwa ,tunajitahidi kulipa , wazazi wameshindwa kulipa bili ya siku za nyuma,hapa kuna maji ya aina mbili yapo ya Ruwasa na mengine yamfeji ndiyo wanatumiwa kwa sasa
Ezekiel Maningo ,kutoka Bodi hiyo ya Magadini Makiwaru amesema haya maswala ya Taasisi wanatakiwa kufika ofisini ,upon utaratibu wa namna ya kufanya kwa hiyo waje ofisini
Idrisa Mndeme mdau wa elimu Wilayani humo,ametoa rai kwa Serikali isaidie kama inawezekana wa kupata yale magari ya kuchimba visima ,angalau kila shule iwe na kisima kimoja kimoja visima kujenga Ustawi wa shule Kwa ujumla
Kwa kweli Serikali imejenga shule nzuri,lakini changamoto ambazo zipo ni maji,shule inashindwa kulipa bili maji yanakatwa changamoto inakuwa kwa wanafunzi kupata magonjwa ikiwamo UTI,wanaanza kwenda hospital kujitibu
Kwa hiyo wito wangu Serikali ichimbe visima kwani ni ya uhakika kuliko hayo mengine wakati mwingine yanakatika ,ukichulia vyoo vinavyotumika ni vya kisasa vinahitaji maji muda wote
Mwisho